Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

Maneno meeeeengi na ngonjera hakuondoi definition ya Uzalendo.

patriotism
ˈpeɪtrɪətɪz(ə)m/
noun
noun: patriotism
the quality of being patriotic; vigorous support for one's country

Huwezi kuwa mzalendo kwa nchi isiyo yako. Askari wetu kwepo Congo, hakumaanishi wao ni Wazalendo wa DRC, NO. Christian Bella anaweza kuipenda Tanzania, lakini hawezi kuwa mzalendo kwa nchi yetu. Hawezi kuipigania Tanzania dhidi ya nchi yake, na hapo ndio maana ya uzalendo inapatikana.
 
Mkuu hujanijibu bado .nitajie wimbo wa afande sele wa peke yake mkali/uliohit ambao hata leo unaweza ukausikiliza na ukakukonga moyo.
 
Uzalendo ni kuipenda NCHI yako na kuiunga mkono siku zote wakati wowote, pia ni kuiunga mkono SERIKALI yako kwenye mambo ya maana.

Kuiunga mkono serikali muda wowote sio uzalendo hata kidogo. Kuikosoa pale inapokengeuka ni moja ya majukumu ya mzalendo.
 
ni kwel uzawa co hoja lakini inauma Kuwaacha wazawa sababu ni nyimbo ya Tanzania na co Africa
 
Mimi ni Adui no.1 wa Sera za ccm, Lakini kwa Hii LA uzalendo na maana halisi ya Uzalendo Mpoto Ameongozwa na Akili kubwa na Hekima ya Hali ya Juu sana Huyo Afande nadhani Bangi zimemuathiri sana, Uzalendo Ingekuwa ni uzawa Leo Tusingepeleka Askari wetu Kongo tungewaacha wakongo wauane wao kwa wao Uzalendo ni zaidi ya uzawa
 
Hiyo inategemea na wasanii wa nchi husika
 
kama ni kuhamasisha uzalendo kwa Taifa ..basi ni vema wazawa wawe kipaumbele lakin yote 9 .......10 mbona sioni kama ni sahihi kwa hawa watu tena watanzania kujibishana kwenye mitandao ya kijamii.Mbona wanaweza kuwasiliana private na wakarekebishana mitazamo yao pasipo kuleta picha ya kutoelewana baina yao..ushauri wangu tu kwao wawe watulivu...wakutane wawili wawekane sawa .......
 
Hapa umenena mkuu nasubilia mwingine aniweke sawa maana😵😵😵😵
 
Kuna kipindi wamarekani walitaka Obama asichaguliwe kwa sababu sio Mmarekani.
Hapa unasemaje!
 
Mrisho amejikita kwa pfof Shivji na mifano ya kina Okello katika kuonyesha uzalebdo. Lkn bado mjadala unaweza kuendelea kwamba ni kweli wazawa wameshindwa kuwa wazalendo mpaka wapatikane wageni? Mie namuona Mrisho amekimbia hoja ya msingi hapa. Katuhumiwa kumtowa mzawa na kumuingiza mgeni je kafanya kweli hivyo au hakufanya? Badae ndio tuendelee na ngonjera za kina Okello.
 

Sawa mkuu kama marekan wenyeji ni red indians pekee sisi hapa kwetu wangoni wametoka south,wamasai ethiopia,pia kuna wamalawi,waha wamtoka burund wahaya uganda wamakonde msumbiji tunawajaluo pia uzawa ni ubinafsi na ubaguz nasisitiza fatilia historia ya africa na historia ya wabantu sis hatuna tofaut na marekan
 
Totally wrong, wewe na huyo Mrusha Mpotoshaji. Askari wetu walioko DRC sio Wazalendo wa DRC. Wapo pale kazini tu. Amiri Jeshi wao ni Rais wetu na sio Rais wa Congo. Leo hii Congo wakitukorofisha, hawatapigana upande wa Congo, watakuwa upande wetu kuonesha uzalendo kwa nchi yao.

Huwezi kuwa Mzalendo kwa nchi ya mwenzio, unless you are stupid, lkn unaweza kuipenda nchi nyingine.
 
Kuna kipindi wamarekani walitaka Obama asichaguliwe kwa sababu sio Mmarekani.
Hapa unasemaje!
Hio ilikua hoja ya kisiasa tu ndio maana walimpa mihula miwili they dond give a damn about where you come from ila utafanyanin?
 
kwahicho alichokijibu mpoto nahoja za ushahidi wake alizozitoa nampa..tano katisha
nampnda afande sele yule mwenye mitazamo chanya wakipindi cha mkuki moyoni...lakini hapa amefeli..hata Michael Jackson alimuimbia msichna wakiliberia wimbo nakuitukuza Liberia sio kwamba America ilikuwa imeishiwa warembo...Bob Marley nae alituasa Africa kuungana nakuwa kitu kimoja sio kwamba yeye alikuwa niraia wkutoka Africa..tena akashindilia msumari wamwisho kuipamba Zimbabwe ktk tungo zake murua...
afande sele alikuwa sahihi alipotoa mtazamo wake juu ya kanumba dhidi ya lulu...
ila hayupo sahihi ktk hili ..yeye anajuaje labda Bella tayari keshapewa uraia wanchi hii..

then unapokuwa nahekima nabusara kunamambo mengine unastahiki kuynyamanzia kimya hata kama nimabaya.. lakini kwakuwa haywezi kukudhuru hugeuka nakuwa sawa najema lisilo nafaida
 
Mkuu hujanijibu bado .nitajie wimbo wa afande sele wa peke yake mkali/uliohit ambao hata leo unaweza ukausikiliza na ukakukonga moyo.
watu na Pesa ..mkuu nibonge ya ngoma..
 
MPOTO YUKO SAHIHI ILA KWA TAHADHARI



KWA MFANO
IKITOKEA MGONGANO WA MASLAHI KATI YA DRC NA TZ, CHRISTIAN BELA ATAKUWA TAYARI KUTUMWA NA DRC DHIDI YA TZ ILA HAWEZ KUTUMWA NA TZ DHDI YA DRC.

NADHANI NIMEELEWEKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…