Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 412
Ukiniuliza nani anafaa kuwa rais wa Tanzania 2015 nitasema ama Mpina, au Lisu,au Lema. Nawatazama viongozi hawa vijana kama alama ya mabadiliko kwa ustawi wa taifa letu. Viongozi hawa wapo wazi na wala hawana chembe ya unafiki. Ujasiri wao ndani na nje yabunge naweza kuiita ni asilia (in-born), si kama baadhi ya viongozi wengine vijana ambao wana ujasiri wa kutengezezwa. Mfano wa hawa ni Makamba Jr, Mnyika, Filikunjombe, n.k... Kwa upande wangu ningefurahi kama Mpina atakuwa rais wa Tanzania. Naona wivu sana nikiangalia safu ya viongozi wakuu wa Kenya, akina Uhuru, Rutto, nk wote vijana. Kwanini hapa Tanzania tuendelee kung'ang'ania kuongozwa na wazee kama Kikwete, Slaa, Lowasa, Membe, Sita, Wasira! Tumekosa nini sisi vijana?