Nani zaidi kati ya Edo Kumwembe vs Shaffi Dauda


Aisee liki abdallah ni shabiki mkubwa wa Liverpool na Simba ingawa mpira wa ndan yeye si mpenz sna na ki ukweli huyu ndiye mchambuz wa soka la nje mwenye upeo wa aina yake ingawa eddo is bright pia na uzur wa eddo uko zaid kwenye sanaa ya Uandishi ingawa ukiwa msomaji wa mtandao unaitwa Eurosport utakuta kuna makala kadhaa anaiga usanifu kdgo tho anajitahid kuweka knowledge yake.
Wanaoponda kuwa hawa jamaa wanatoa habar kweny mitandao ya kimataifa nawashangaa kwasababu unategemea mtu kama eddo atafunga safar kila siku barnebeu, au carrington akitafuta habar? Ukweli ni kua hawa wako so ordinary kipya watakacho kupa ni habar za kina samatta na JKT Ruvu angalau eddo ameonyesha ukomavu wa kwenda Naples kufanya interview na mariga lakini take a look ya financial muscle yake na kampuni anayofanyia kaz wataweza mara ngap kumpeleka uko? Hata vyombo vikubwa vya habar kama Sky Sports na Soccernet wanafanya refference ya vyombo vingne mfano magazet km The Sun, Daily Mirror etc. Binafsi sion tatizo wakifanya refference ila tu isiwe copy n' paste iwe kama vile Dr. Liki alivokua ana dadavua mana hata yy alikua anachukua habar za mitandaoni ispokua alikua anaongezea na ka weled kake hasa kwenye technical issues.
 
babumapunda ni vigumu kupambanisha mtu wa print media (Edo) na mtu wa electronic media (Shafii),kitaaluma wote ni waandishi wa habari lakini kiutendaji Wako tofauti sana.

Mkuu linapokuja suala la uchambuzi wa soka nadhani tunaangalia uwezo wa kiufundi zaidi wa mchambuzi kuliko aina ya media walizopo.
Bado sijaona uchambuzi wowote wa Shaffih kuelezea/kukosoa na kushauri Ufundi wa kabumbu
 
Last edited by a moderator:
Jamali Malinzi, heshima yako mkuu
Umekoment vzr but kama unavyosema kiutendaji wako tofauti sana hiyo tofauti ndo binafsi nahitaji kuijua

babumapunda ni vigumu kupambanisha mtu wa print media (Edo) na mtu wa electronic media (Shafii),kitaaluma wote ni waandishi wa habari lakini kiutendaji Wako tofauti sana.
 
Last edited by a moderator:

Acheni hizo za kutafuta kwenye google, kuna ladha ya kusimuliana na kuulizana hata kama unajua unaweza pata hiyo taarifa google!

Kwa nini tunaanzisha thread ya mechi za habari kutoka kwenye mitandao mingine ya nje badala ya kuweka link tu? Au ukasema katafute website fulani.

Kwa nini tunaanzisha thread za mechi ambayo sote tuko tunaiangalia?

Kwa hiyo watafsiri wataendelea kuwa muhimu hata kama anacopy paste.

Back to the topic:-
Edo anaweza kuja kuvaa soksi (viatu hataweza) za mkuu Riki Abdallah. Riki alikuwepo kabla hata watu wengi hatujaanza kupata access za internet na ladha yake mpaka leo inatachi ileile.
 
Mpaka naandika hii comment Edo anaongoza kwa 100%, au?

Maana sijaona hata mmoja aliyesema Shafii ni zaidi ya Edo.

Walio challenge wamesema wote sio au wako sawa.

Edo Bingwaaaaa!
 
Mie nanunua gazeti la mwananspoti kwa ajili ya Edo Kumwembe, pia nasikiliza Spoti Extra iwapo tu anatangaza Luambano nikisikia Maestro nazima redio, pia nampenda Shaffi kwa kuwa ni mjasiri anahoji vitu particularly TFF. Ila Edo yuko juu zaidi
 
soma alichoandika kwa makini utagundua iq yake ilivyo ndogo, kama hutaona basi mko na same level of thinking

This is defensive.

Kwa jinsi ulivyo jibu ni dhahiri umekosa justification na kutafuta njia ya kutokea. Kwa kufanya hivyo, umejishusha wewe zaidi na kumkweza yule uliyetaka kumshusha.
 
wakuu nimeamua kuleta uzi huu kwenu ili kutaka kupima kati ya wachambuzi hawa mairi wa Soka nchini ni yupi mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua soka la Nchini na nje ya nchi.

ni hayo 2,karibuni kwa kuchangia.

Edo kumwembe yupo juu zaidi ingawa anapenda sana kumsifia samatta sijui kwavile dogo akijaga anamletea vitisheti na raba
 
Mimi naona wote ni sawa katika umahiri wa kuchambua habari za michezo za ndani na za nje, wanachambua habari hizo kwa kina na weledi. Sema tu umahiri wao ni katika kuwashawishi wasomaji wao wanachotaka wao, siyo inavyotaka taaluma. Wanatakiwa wajenge tabia ya kutuchambulia habari kwa kadri akili zao zinavyobaini, siyo kwa kadri mioyo yao inavyowatuma. Angalau ingekuwa wanatumwa na mioyo yao, ingekuwa bado afadhali. Nina wasiwasi wanatumwa na watu wengine wanaowajua wao, kwa mslahi ya hao watumaji. (Kwa bahati mbaya hivi ndivyo walivyo 'wachambuzi wetu wote, wa habari zote).
 

umeongea point nzuri sana! Nashangaa wabongo wanavyoponda mtu kutoa habari kwenye mtandao! Sijui walitaka azipate wapi? Awe kila siku anapanda ndege kwenda old trafford???? Dhambi ni ile kuitoa kwa audience bila kuidadavua kwa kuongeza weledi wako...
Anyways, edo is better than shafii
 
NI dhahiri Edo ni bora lakini si kwamba Shafii hafai. Katika vitu vilivyobora kuna kimowapo ni bora zaidi. Lakini wote wawili kwa maoni yangu wanayo matatizo. Ya kibinadamu kabisa. Uchambuzi wao mara nyingi unagubikwa na ushabiki wa timu zao. Katika uchambuzi wa soka la ndani, Edo haikosoi Simba kwa namna ileile anayoikosoa Yanga. Sina taarifa rasmi, lakini nikiangalia uchambuzi wake, napata hisia kuwa yeye ni Simba damu. Shafii kwa kiwango kukubwa ni hivyo hivyo.
kwa upande wa uchambuzi wa soka la nje, Edo yupo juu zaidi. Anajitahidi kusoma vianzo Tumbalimbali. Kila anapochambua soka la Latin America, utaona dhahiri jinsi anavyo toa vitu kwa Tim Vickery wa BBC - Idara ya soka la Amerika Kusini. Sijaona kama Shafii kama anachmabua zaidi ya ku copy and ku paste. Edo ana copy, anatafsiri, anaongeza yake na kulinganisha na sehemu nyingine angalau.

Tusisahau kwamba mmoja anaandika uchambuzi wake. Unapata nafasi zaidi ya kurejea tena na tena maoni yake, Mwingine nin mtangazaji, unayasikia yanapita. Hapo kuna tofauti kubwa sana.

Zaidi, inaonyesha Edo pamoja na uchambuzi, anaujua mpira - mifumo, aina ya wachezaji nk.
 
wako equivalent yan edo ana degree shafii ana advancedipolma.
Tatizo la shafii n mwanasiasa wa mpira.JeFUU anajitahd atakuja kuwa bora badae tena zaid ya Shafii.
Ila baba yao n Dr Liki huyu n master
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…