Nanjumba, Lindi: Shule shikizi yakosa Mwalimu tangu mwaka 2021, Wanafunzi wa chekechea hadi darasa la pili wakosa Masomo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakazi wa kitongoji cha Nanjumba kata ya Likawage wilayani Kilwa mkoani Lindi walipokuwa wanazungumza na Mashujaa FM wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa mwalimu katika shule shikizi iliyopo kijijini hapo tangu mwaka 2021 hali inayopelekea wanafunzi wa chekechea hadi darasa la pili kukosa masomo.

Wakazi hao wameeleza kuwa bado kuna muamko mdogo wa viongozi wa halmashauri ya Kilwa kutembelea shule hiyo ili kujionea changamoto zao, licha ya majengo ya shule hiyo kujengwa kwa nguvu ya wakazi wa kitongoji hicho na msaada wa fedha za mfuko wa jimbo na mfuko wa kijiji kwa lengo lakutatua kero ya watoto kutembea umbali mrefu wa takribani kilomita 8 kwenda shule ya msingi Likawage.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Geofrey Jafari amesema shule hiyo haijasahaulika na wanatambua changamoto ya kutokuwepo kwa mwalimu katika shule hiyo, ambapo kwa sasa wana mikakati ya kupeleka mwalimu mwingine na amewataka wananchi kuwa na subira kwani halmashauri yao inalifanyia kazi suala hilo.

Chanzo: Mashujaa FM
 
Likawage nimefika huko ndio maangamiz ya tembo hufanyika kuna njia inaenda had Kijiji Cha nanjilinji

Jiogragia ya kilwa ndyo inayotesa wafanyakaz wengi hukimbia maeneo hayo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wakazi wa kitongoji cha Nanjumba kata ya Likawage wilayani Kilwa mkoani Lindi walipokuwa wanazungumza na Mashujaa FM wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa mwalimu katika shule shikizi iliyopo kijijini hapo tangu mwaka 2021 hali inayopelekea wanafunzi wa chekechea hadi darasa la pili kukosa masomo.

Wakazi hao wameeleza kuwa bado kuna muamko mdogo wa viongozi wa halmashauri ya Kilwa kutembelea shule hiyo ili kujionea changamoto zao, licha ya majengo ya shule hiyo kujengwa kwa nguvu ya wakazi wa kitongoji hicho na msaada wa fedha za mfuko wa jimbo na mfuko wa kijiji kwa lengo lakutatua kero ya watoto kutembea umbali mrefu wa takribani kilomita 8 kwenda shule ya msingi Likawage.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Geofrey Jafari amesema shule hiyo haijasahaulika na wanatambua changamoto ya kutokuwepo kwa mwalimu katika shule hiyo, ambapo kwa sasa wana mikakati ya kupeleka mwalimu mwingine na amewataka wananchi kuwa na subira kwani halmashauri yao inalifanyia kazi suala hilo.

Chanzo: Mashujaa FM
Daahhh!Kazi ipo
 
Back
Top Bottom