Nanunua nguo kila ninapokutana na machinga hata kama sizihitaji, nifanyeje kuondokana na tabia hii?

Hapana sio sahihi. Kwa kazi ninayofanya nguo za kazini ni special kwaajili ya kazi. Mara nyingi Hua nashindia za kawaida.
Basi wenzako nguo anashindia Jumapili home, Jumatatu anaamkia nayo kazini.
Sema Jumamosi tunajiachia sana makazini.
 
Kuna nyumba niliingia yule kaka ana viatu nahisi pea 100 zinafika. Nae akadai kama wewe hivyo hivyo akifika mahala akaona kiatu kizuri ananunua awe anauhitaji au la ilimradi kimemvutia anabeba.
 
Zamani nilikuwa chizi kama wewe, lakini sasa hivi sioni muhimu tena kununuanunua kama wewe,
Mwaka jana nilipaki mizigo kwenye shangazi kaja kwa ajili ya kijijini, bado nitafanya hivyo tena mwaka huu.
Nataka nibaki na pea 10 ya kila kitu, japo ukiwa na mzigo mkubwa unavaa tu.
Jifunze kutembea na pesa kidogo kwenye wallet. Sio kila unachoona unanunua, ukiwa Bar wakipitishapitisha jifanye huwaoni.
 
Kua na nguo nyingi sana sio kitu kibaya kwa sababu inafanya unakua na options nyingi na unakua huchakazi nguo kwa sababu unaivaa mara chache ndani ya muda mrefu. Muhimu tu ni kuhakikisha unanunua nguo nzuri kweli kweli ili usije jikuta unakua na nguo nyingi ambazo hazieleweki
 
Hivi Tanzania kitu kama hichi hakijafika hadi zama hizi?


Ni wakati sasa watu waanzishe vitu kama hivyo kuondoa kadhia ya kitu/vitu usivyokuwa na uhitaji navyo tena basi jua kuna mtu/watu wana uhitaji navyo sio vya kutupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…