Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 11,936
- 15,196
Wakuu Salam,
Nipo wilayani Nanyamba huku kusini maisha ya wananchi kiuchumi yapo hoi sana. Wilaya ya Nanyamba hutegemea korosho pekee kama zao la biashara. Hata hivyo kabla ya 2017 zao hilo liliweza kuwa mkombozi wao kiuchumi. Mwaka 2017 serikali ya CCm bila kufanya utafiti wa kutosha waliingia kwa kutumia majeshi ununuzi wa zao hilo. Hali hiyo ilipelekea kushuka kwa bei kwani wanunuzi wengi kupitia makampuni yao walijiondosha kwenye mchakato wa ununuzi wa zao la korosho.
Hivi ninavyozungumza hapa watu wameshindwa kabisa kuandaa mashamba na hawajui hatima yao.katika msimu uliopita kile ilikuwa 1500/=. Kuonesha kuwa hali za wananchi zipo duni kiasi cha kukosa chakula walilazimika kula embe kama chakula kipindi cha msimu huu wa mambo.
Wanamuomba mama Samia aliangalie zao la korosho kwa jicho pana Keanu ndiyo mkombozi wao.
Alamsiki.
Salam toka Nanyamba.