Naogopa kuchukua/withdraw pesa kwenye bank account yangu

ze meck

Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
36
Reaction score
6
Natumaini wanajamvi ni wazimaa wa afya

Kama mada ilinavyojieleza ..Mimi ni mjasiriamali mdogo. Nimekuwa nikifanya biashara ndogo ndogo baada ya kutoka shule.

Muda mfupi uliopita niliingia kwenye matatizo na familia yangu ki ukweli nilivyurugwa kisaikolojia..hela cash iliyokuwapo mfukoni nilimaliza kuila...Nikauza kiduka ambacho nilimfungulia mke wangu nacho hela imekwisha bila kujielewa...Nilikuwa na kiduka changu binafsi nacho kimekwisha

Hapa Majuzi nimeuza pikipiki yangu basi ile hela nikaiwe Bank kwenye saving account..

Leo nimeamua kurudi kwenye bussiness lakini nasita kuchukua hela kwenye account yangu ili nirudi kibiashara..sijajua kama bado kisaikolojia sijakaa poa....au uoga wa kuishiwa


Msaada jamani please

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole sana....Ila ungeeleza kitu kilichokuvuruga na familia ili tukushauri kulingana na hali iliokuepo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani lengo la kuuza pikipiki ilikua nini? matatizo huja na kuondoka usikufe moyo rudi tena kwenye Biashara. matatizo yakirejea chunga sana usikule mtaji kwani itakugarimu sana kuupata na kurejesha Biashara yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…