Naogopa sana kuomba msaada; Kwangu kukwama si jambo la kawaida

Nachofanya ni kujaribu kadri niwezavyo nisifikie huko kwa kujijengea mfumo mzuri, mwanzoni inaweza kukutesa ila ukiweza kui master unaishi kwa amani zaidi ya wale wanaoona kukwama au kuomba msaada kila mara ni jambo la kawaida
Staili hii ya maisha haijawahi kua na amani hata kidogo mkuu zaidi ya hofu.

Acha uoga Maisha si mtihani wa kuonyesha kwamba unaweza kubeba kila kitu peke yako, ni safari ya kujifunza kusimamia ulichopewa huku ukikubali kwamba wewe pia ni binadamu.
 
Nakuelewa mkuu
Sidhani kama nguvu ya mtu inapimwa kwa kutohitaji msaada kamwe. Wakati mwingine nguvu ya kweli ni kujua kwamba umefanya kila uwezalo, na unaposhindwa huna aibu kusema, Nahitaji msaada.

Pia

Kuna wakati kujinyima ni busara, na kuna wakati kunakuwa adhabu unayojipa mwenyewe kwa sababu ya kesho usiyoijua. Kula Bata uiishi Leo yako lakini pia usisahau kuweka akiba kwa kesho yako isiyojulikana
 
Noted Kabisa Boss... Ila Kama Mimi Hapa Nachangomoto Na Sijapata Hata Wakunikopesha 20000 Nitakurejeshea
 
Iwe umewahi kuomba zamani
Au upo kwenye mchakato wa kuomba
Au utaomba huko baadae la
Muhimu ni kujua hakuna msaada wa bure bure

So ukijua kuomba ujue kuna kutoa
Baadhi ya wazazi wenyewe unakuta anakusomesha ili baadae uje umsaidie
 
Iwe umewahi kuomba zamani
Au upo kwenye mchakato wa kuomba
Au utaomba huko baadae la
Muhimu ni kujua hakuna msaada wa bure bure

So ukijua kuomba ujue kuna kutoa
Baadhi ya wazazi wenyewe unakuta anakusomesha ili baadae uje umsaidie
Ni kweli hakuna msaada wa bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…