Naokota sana pesa hadi najishangaa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Habari za mihangaiko wakuu.

Mimi naishi Ubungo kila siku napita njia ile ya Riverside to Makoka. Sasa haiwezi kupita siku tatu bila kuokota hela, mara nyingi ni 200 na 500. Kwa mfano leo asubuhi nimeokota 200 mara mbili halafu maeneo tofauti, jana pia nimeokota 500 japokuwa jana nilimuona mdada aliyeiangusha ila nikaiokota kimyakimya.

Kifupi kuokota hela kwangu ni matukio ya kawaida sana, sasa najiuliza hii bahati inatokana na nini? Au kwa sababu nazurura sana na ni kweli me huwa natembea sana sometime sipand daladala naamua kufanya mazoezi njian nakutana na mazali kama hayo kuokota hela.yaani hadi raha

Kwenye kucha karibu vidole vyote nina vile vialama vya madoa meupe
Wana jf wenzangu nipeni maoni,pongez au ushauri
 
Usifanye kazi yoyote wewe endelea kutembea barabarani kwa miguu kuna siku utaokota begi au gunia lenye hela za escrow na utakuwa tajiri
 
Usifanye kazi yoyote wewe endelea kutembea barabarani kwa miguu kuna siku utaokota begi au gunia lenye hela za escrow na utakuwa tajiri
Pia nimegundua unapotembea style nzuri ni kuinamisha kichwa chini.sio muda wote shingo pembeni hapana nikitembea natazama sana chini naangaza huku na huku
 
Pole sana mkuu. Ila usiifanye ndio tabia kwa sababu hakuna tabia mbaya kama ile ya kutegemea nitapata kitu fulani pasi kukihangaikia.

Kuwa makini sana kwa sababu unaweza tembea usikutane na hela njiani na ndio itakuwa mwanzo wa kuwaza kukwapua ili tu upate chochote kitu kwa sababu hakuna aliyedondosha.
 
Umemuona aliyedondosha ukaokota[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kumbe kuokota hela definition yake ipo tofauti siku hizi
 
Waswahili tuna msemo wetu, ya kuwa mtembea bure si sawa na mkaa bure, huenda akaokota. Kwahyo wewe endelea kutembea kwani utazidi kuokota kwa wingi.
 
Mna majibu mabay.mbona roho mbaya hivi..sasa maada hapo ni uokotaji wa hela we unaleta pumba
Weka utaratibu wa kupita maeneo ya benki muda wa jioni unaweza ukawa unaokota za noti noti kwa wingi sana, pia usisahau kupita berau ukalokota ma madolari pia.
 
Mkuu okota za nauli hizo unaonekana unatembea sana punguza kula miguu ya kuku hufanya watu kutembea sana.

Anza kula vichwa vya kuku vinasaidia kuongeza akili kama za kuku.
 
Davido aliimbaga "money follow you, banana follow you"
Ukiona hela zinakufata hivyo basi jiandae kwa banana(dudu washa).
 
Na wewe ukitupa zako ujue zinaenda kwa wenyewe ulizookota
 
Pia nimegundua unapotembea style nzuri ni kuinamisha kichwa chini.sio muda wote shingo pembeni hapana nikitembea natazama sana chini naangaza huku na huku


hizo ni hela za makafara...na ushafanywa kama li-swagi

hushituki kijana mzima kuinamisha bichwa chini...njia nzima,unatafuta...100,200..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…