Jamanieee, samahanini, pamoja na kwamba nitakuwa naiba haki miliki ya watu, naombeni kama kuna mtu mwenye ramani za kujenga nyumba, yaani design za nyumba, muwe mnatuwekea hapa tuweze kudownload ili tujenge nyumba zetu nzuri. kama kuna mtu anayeweza akatuwekea hapa aina ambazo zitatufaa kwa weather ya hapa tz, nitashukuru. asanteni.
Ndugu yangu Mbeba Maono,
Kama walivyoshauri watu wengine, nitaongezea kwa kusema kuwa ni vigumu kupata nyumba inayoweza kukidhi matakwa yako kwenye internet.
Kuna vigezo vingi vya kuzingatia kabla hujapata nyumba inayokidhi matakwa yako. Baadhi ni hivi hapa:
Sehemu ambayo kiwanja chako kipo:
Kwa mfano ramani ya nyumba inayotakiwa Sinza ambako tayari nyumba zingine zimejengwa na huna nafasi ya parking na fensi haiwezi kufanana na ile itakayofaa Boko ambako una eneo la kumwaga.
Kiasi cha hela ulizo nazo.
Uwezo wako pia unachangia kujua aina ya nyumba inayokidhi matakwa yako.
Mazingira ya kiwanja chako,
kama kipo mlimani, tambalale, au kwenye mpomoromoko, au kwenye ardhi ngumu au kwenye majimaji kama Jangwani, sababu hizi zitachangia aina ya design ya nyumba inayokufaa. Kuna viwanja msingi tu unaweza ukala hela zako zote ulizonazo.
Hizi ni baadhi ya sababu chache zinazosababisha nyumba zisifanane, ukichunguza sana hata maghorofa yetu yanayoanguka unaweza ukakuta ni kwa sababu wahusika hawakuweza kufanya utafiti wa kutosha wa aina ya nyumba inayofaa kwenye kiwanja husika.
Ukitaka usaidiwe zaidi weka maelezo kamili ya kiwanja chako hapa pamoja na picha yake nina imani JF inakila aina ya watu including clazy architects ambao wanaweza kukusaidia, (though I am not sure if somebody can offer his service at free of charge, anyway try your lucky) kama uko Dar basi kama walivyoshauri wengine nenda kwenye Board of QS & Architects utasaidiwa zaidi.
Lakini ile tabia ya kusema hii ramani ninaipenda na ndio hii inanifaa inaweza isifae kwenye mazingira ya kiwanja chako. Hebu tubadilike na tujenge tabia ya kuwatumia watalaam wetu tuliowasomesha kwa pesa za wakulima na wafanyakazi. Ukipata ramani inayokufaa wasiliana na mimi nikupe gharama ya nyumba yako; However, consultancy will be at cost.
Nsaliwe Njimba
Construction Economist.