Mkataba ni zao la matakwa ya wahusika katika mkataba na Mahakama kazi yake ni kutafsiri malengo ya wahusika na kulinda maslahi yao ndani ya mkataba.
Hata hivyo,Mahakama katika kutafsiri Mkataba inatikiwa kuzingatia sheria za nchi,taratibu na kanuni za kisheria zinazojulikana.
Hata hivyo ndani ya mkataba kunaweza kuwepo na kipengele ambacho kwa taathira yake kina maana kubwa zaidi ya ile inayoonekana wazi.
Nirudi kwenye maswali yako.
(1) Hapo awali nilisema kuwa lengo la dhamana si kuhamisha umiliki wamali ya mkopaji kwenda kwa mkopeshaji bali lengo ni kulinda mkopo.Hii ni kanuni ya kisheria inayotawala mambo ya mikopo inayoambatana na dhamana (Mortgage ).Kanuni hii haipo kwa ajili ya kuzuia haki za Mkopeshaji lakini ipo kwa ajili ya kulinda dhamana.
Dhamana inatakiwa kuuzwa baada ya mkopaji kushindwa kulipa mkopo,hii ina maana tarehe ya mwisho ya kulipa mkopo inaweza kuzingatiwa na Mahakama katika kutoa amri ya kupiga mnada dhamana.
(2)Hakuna sheria inayomzuia mkopaji kwenda kokote atakako na wala hatakiwi kumuomba ruhusa au kumtaarifu Mkopeshaji mahali anapokwenda,dhamana yake ndiyo ulinzi wa Mkopeshaji.
No consultation fee