Naomba Kazi ya online

Naomba Kazi ya online

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,692
Reaction score
5,647
Natumaini mu wazima wa afya.

Natafuta kazi ya online.

Si kwamba hata ya kufika eneo la kazi siiwezi,bali jukumu limetaiti sana.

Kwa sasa nipo na watoto wawili wadogo,na kila kitu kuhusu wao ni mimi tu. Hapo nyuma kidogo mambo yalienda ovyo, mama yao akaamuwa kuwaacha. Ni bado wadogo,miaka mitatu kasoro.

Nimejikuta nalazimika kuanza maisha upya nikiwa nao. Hivyo, kuweza kumlipa msaidizi,bado.

Nina kazi ya online inayoniwezesha kidogo kuwasogeza,ila kusema ukweli bado. Mi baba,mama, msaidizi, kila kitu.

Mahitaji yao ni mengi,Na wakiugua ni balaa; hata ya kinyumbani kujipanga,bado miezi kadhaa kuweza kukaa vizuri.

Kama kutakuwa na mtu anahitaji tafadhali naomba aniboost niweze kuwatunza.

Nimepambana, na bado napambana,ila kusema ukweli, kulea si kazi ndogo.

Kina mama wenye mapenzi na watoto wenu,mpewe maua yenu.
 
Aina gani na una ujuzi gani mkuu

Online kuna Kazi nyingi ungesema moja unayoipenda kwanza.
 
Aina gani na una ujuzi gani mkuu

Online kuna Kazi nyingi ungesema moja unayoipenda kwanza.
Duh! Kwa sasa nayofanya,ni content creator. Mi nimesomea mambo ya IT, ngazi ya certificate tu. Ila uzoefu,ndo nilionao wa kutosha(biometric devices,maintenance,networking,cctv, electric fence,.....). Na hizi kazi huwa si za online,lazima uwe eneo la kazi. Kwa hiyo,yoyote ikiwa nje ya ujuzi,nikielekezwa nafanya.
 
Hao watoto ungewapeleka kwa bibi yao! Lakini kukaa nao mkuu bado ni changamoto mwanaume kukaa nyumbani ni kazi kweli kweli kazi za online labda uwe na channel yako ya youtube inayokulipa na yenyewe itabidi utoke ukatafute content! Bila kutoka nje kufanya kazi utaendelea kuumia
 
Hao watoto ungewapeleka kwa bibi yao! Lakini kukaa nao mkuu bado ni changamoto mwanaume kukaa nyumbani ni kazi kweli kweli kazi za online labda uwe na channel yako ya youtube inayokulipa na yenyewe itabidi utoke ukatafute content! Bila kutoka nje kufanya kazi utaendelea kuumia
Nakuelewa ndugu. Lakini kumbuka,siku hizi watu wengine hawataki mizigo isiyo ya kwao. Mpaka naamua hilo,ujue kuna majalibio mbali mbali yaliyosababisha kufikia uamzi huo. Pia,watoto kama wamekosa mapenzi ya mama, kuna mtu mwingine atawapenda zaidi? Ni wangu,siwakatai. Najua nahangaika,ndo ilivyo,lakini mimi ndo naejua waliyoyapitia. Bado najitafuta angalau kuweza kumlipa msaidizi,ndo ntaweza kutoka na kutafuta.
 
Back
Top Bottom