Naomba kuelekezwa jinsi ya kuhifadhi mafuta ya nguruwe yasiharibike

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Baada ya kuona wataalamu mbalimbali wakishauri tutumie zaidi mafuta ya kupikia yatokanayo na wanyama badala ya mbegu nimeona mafuta ya nguruwe yatanifaa. Nimepata wazo la kwenda kuyanunua buchani na kuyatayarisha kisha kuyahifadhi. Sasa ninaomba kwa anayefahamu namna nzuri ya kuyahifadhi ili yasiharibike.

KARIBUNI
 
Hayo mafuta siyapendi kishenzi kuna sehemu nilienda kutembelea wakawa wanapikia hayo mafuta ya kitimoto na mafuta ya mawese pekee chakula sijui nilikua nakionaje

Kuhifadhi unaweka kwenye chupa tu km mafuta mengine hayaharibiki
 
Baada ya kuona wataalamu mbalimbali wakishauri tutumie zaidi mafuta ya kupikia yatokanayo na wanyama badala ya mbegu nimeona mafuta ya nguruwe yatanifaa. Nimepata wazo la kwenda kuyanunua buchani na kuyatayarisha kisha kuyahifadhi. Sasa ninaomba kwa anayefahamu namna nzuri ya kuyahifadhi ili yasiharibike.

KARIBUNI
Katakata vipande vidogo kama nyama ya kupika vile. Chemsha mafuta hayo bila maji kwani yatajikaanga kwa mafuta yake yenyewe. Chemsha hadi mafuta yote yatoke na kuwa na rangi ya brown kama nyama iliyokaangwa. Epua mafuta yaache yapoe kidogo.

Waweza kuondoa mabaki au kuyaacha ndani ya mafuta. Hizi ni kama nyama zilizo kaangwa ni tamu sana. Hifadhi mafuta yako kwenye chombo safi na ufunike vizuri. Usihifadhi mafuta yoyote kwenye mwanga kwani huharibika mapema. Kwa namna hii mafuta yako yanaweza kukaa ha miaka 3.
 
Asante sana ndugu
 
Back
Top Bottom