Naomba kuelekezwa lodge ambayo naweza kulala maeneo ya Manzese

Naomba kuelekezwa lodge ambayo naweza kulala maeneo ya Manzese

Kaka lodge za manzese walinzi wenyewe ndio wezi. Kuwa makini unapoweka suruali na mabegi,wanaiba hela tu vingne wanakuachia. Me nililala midland ghorofa ya kwanza lakini wakanichapa 25000/= hapo. Ipo road tu
 
Jaromax tip top 50K min room hutojutia, very cool, club na bar viko juu kabisa very cool pia.

Silver paradise tip top pia 35K min hutojutia, very cool, hakuna club ila kuna cool bar...

Erado tip top pia unapata kwa 35K mini shida makelele live band pale bar......

Hizo ndio standard nizijuazo japo tip top na Manzese yote mpaka mabibo kuna lodges nyingi sana nzuri sana na za kawaida kwa bei ndogo inategemea unapenda nini...
 
Naomba husika na mada apo juu naomba mwenye uzoefu anipe jina la lodge nzuri maeneo ayo isizidi 25 jamani sina hela bajeti yangu ndogo natokea pemba naitaji kukaa apo kwa siku 4 ila ninaemfata yupo na chumba kimoja tu.

Naimani mutanisaidia
Kintunku Guest House tsh 3000 kwa siku
 
Kama upo mwenyewe haujaolewa na hauna mtoto niambie Uko wapi nije nikupeleke ya 25,000/= na wanatoa offer uchague kitu kimoja kat ya breakfast bure, Chips kukuz, pizza [emoji487] au offer ya kulala siku 1 bure ila kama upo peke yako tu
 
Inawezekana mwenyeji wake ni wale watu ving'ang'anizi ambae hata kama ana chumba kimoja na anaishi na familia bado atataka ukimtembelea na wewe ulale hapo hapo! So dada Maryam ameamua kujiongeza ashukie loji ili hata mwenyeji akimng'ang'ania aseme tayari ameshalipia chumba...

Sasa mwenyeji wako ameshindwaje kukuelekeza mpaka uje kuulizia huku?

Ila mi mawazo yangu ya kishetani ni kwamba dada anakuja kwa "njemba" ambayo hawajawahi kuonana (huenda wamekutana jf😉) sasa ili asiliwe kimasihara anataka ashukie loji kwanza "apime upepo". Akiona jamaa analipa ndio ahamie kwake..🤪
 
Naomba husika na mada apo juu naomba mwenye uzoefu anipe jina la lodge nzuri maeneo ayo isizidi 25 jamani sina hela bajeti yangu ndogo natokea pemba naitaji kukaa apo kwa siku 4 ila ninaemfata yupo na chumba kimoja tu.

Naimani mutanisaidia
Uwanja wa Fisi
 
Sogea mbele kidogo hadi friends corner,shukia kituo hicho kuna lodge ya ghorofa inaitwa jumba la dhahabu,room ni elf 15 tu na ni self,full AC
 
ww kama unashindwa kunijibu acha tu mbona unafanya mambo kama sisi tunaosafika tumbo kila mwezi achia izo kakangu
Basi yaishe mrembo Jana kichwa changu hakikuwa sawa nakuja PM kukupigia magoti kabisa!
 
Back
Top Bottom