Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Wataalam wa lugha na historia ya Afrika Mashariki naomba kueleweshwa, ilikuwaje Kiarabu kikaathiri lugha ya Kiswahili kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na lugha za jamii nyingine ambazo tulichangamana nazo toka enzi hizo eg jamii za wahindi?
Na ilikuwaje tukachukua misamiati ya Kiarabu kuelezea vitu/ hali/ ambazo waswahili walikuwa nazo hata kabla ya ujio wa wageni? . Kabla wahindi hawajaja hatukuwa na kachori ndio maana tukachukua neno kachori kutoka kwao, wazungu walituletea shule ndio maana hata hilo neno shule tumelichukua kwao, ila kwa Kiarabu tumechukua maneno ya vitu ambavyo vilikuwepo kabla wao hawajaja.
Kwa kumbukumbu zangu, mwalimu wangu wa Kiswahili nikiwa sekondari alitueleza kuwa wageni walikuja kwetu wakakuta Kiswahili kipo tayari kwahiyo hata bila uwepo wao Kiswahili kingekuwepo ingawa wageni walichangia kukieneza.
Sasa, kama waarabu walikikuta Kiswahili kipo, kwanini neno bahari tulichukua kwao? Kwamba waswahili walioishi karibu na bahari enzi hizo hawakuwa na msamiati walioutumia kuhusu " bahari"?. Ilikuwaje tukachukua salamu ya Kiarabu " marhaba" ?.kwamba kabla waarabu hawajaja waswahili walikuwa hawasalimiani? Pia kuna misamiati kama haki na hekima, ambayo hatukuhitaji uwepo wa waarabu kwa jamii kuelewa hekima au haki, lakini bado misamiati ya Kiarabu ndo ikachukua nafasi,hata neno ardhi pia tumechukua kwao, sitaki kuamini kama waswahili hawakuwa na neno la kuelezea ardhi kabla wageni hawajaja. Mifano ni mingi siwezi kumaliza yote, ila ningependa kufahamu sababu zilizofanya tukachukua misamiati mingi sana ya Kiarabu kwenye lugha yetu.
Asanteni