Naomba kueleweshwa kuhusu busta za music

Kijana spika nzur za bass ni Opra ila kuzipata origina ni mtihani... Na zina bei kubwam. Kipindi zinaanza kutoka tulinunua 1.5mil kwa box ya twin speakers.. Kifupi unahitaj mixer,equaliser,crossover, kama utapenda pata na compressor.. Ila kupata mziki mtamu nunua busta mbili moja ya 1000-1500wats kwa ajil ya midi na 2000+ watts kwa ajil ya bass kama hauna hio hela nunua busta kubwa moja kama 4500watts itakua poa zaid.. Busta pro ambazo hazinaga tabu na spare zake ni rahic kupatikana na nafuu ni MAX MX SERIES kama zile MX1000, MX2000,MX4500. behringer hiz busta zao mpya zinaitwa euro series ni nzur zinapiga mziki mpaka spika yako unaionea huruma ila ikifa ndo bai bai zinatumia resistor ndogo tunaita za chawa hazina spea.. Mambo ni mengi.. Kama upo interested ni PM au nenda UHURU MUSIC STORE - WAKALA WA OPRA NA CANDY ILA USIJE NUNUA BASS YA CANDY , AU NENDA CITY SOUND,- WAKALA WA FIDEK NA MAKOLOKOLO YOTE YA MZIKI , AU NENDA AGGREY MUSIC STORE- WAKALA WA MORGAN NA MAKOLOKOLO KIBAO.. Kua makini bidhaa za mziki feki ni nyingi.. Kama huna uzoef tafuta mtu mzoef sana wa kukuongoza
 
Asante sana kwa ushauri wako mkuu, zipo kwenye boksi zake zipo mbili mbili pamoja na tweeter zake. hiyo booster ya 1500 au 2000 zinaendaga bei gani kwa uzoefu wako? [emoji120] [emoji120]
 
Simu mimi vifaa vya music huwa nanunulia South Africa, Tz electronics ipo juu sana Tv tuu Curved hizi zinauzwa mpaka tsh 12,000,000 kuendelea si utani huo wakati huku ya 2016 haiwezi zidi 5m au 6million..busta iyo ni kuanzia rand 2000 mpaka 3000 hata 1500 inapatikana ukihitaji ntanunua ntatuma utalipia ukiiona ntamtumia dogo au hata wewe mwenyewe ila mimi mwezu ujao tukijaliwa tarehe 10 ntakua hapo home...kama utashindwa tripu next time iyo hela zidisha na tsh 150 utaweka gharams za kuituma na kodi tunduma...
 
Asante mkuu nikiwa tayari ntakutafta
 
Hivi kuna uwezekano Wa kupata busta ya kusukwa na mafundi Wa kawaida na ikawa na kiwango bora na kudumu?
 
Hivi kuna uwezekano Wa kupata busta ya kusukwa na mafundi Wa kawaida na ikawa na kiwango bora na kudumu?
 
Mfano kwa sasa Mimi Nina spika Bass moja ya Fidek, na mid 2 ambazo ni fidek zile za zamani ambazo spika inaonekana kwenye wavu na JBL. Ninatumia power mixer ya Max ila tatizo mziki hausikiki sana hasa ukiwa mbali kidogo na sehemu muziki unapopiga hata ukiwa umbali Wa m30 tu. Ila ukiwa eneo husika muziki unasikika unatoka sana. Je nn laweza kuwa tatizo? Na je kwa hivyo vyombo nlivyo navyo nikitaka kununua busta ninunue ya ukubwa gani ili nitumie kwa hzo spika zote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…