Naomba kueleweshwa maana ya ndoto hizi?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Sijafahamu kama ninaishi katika hali halisi au katika eneo la kufikiria tu. Kuna tabia ya kuamka saa 8 usiku, saa 6 au saa 9, na sababu ikiwa ni ndoto – iwe mbaya au nzuri – huwa naamka.

Kwa bahati mbaya, ndoto za sasa zimejenga hali ya tahadhari na kunipa hofu kwamba kuna kitu kibaya kinachoendelea katika eneo la kiroho. Mfano, jana na juzi nimeota nakula ndotoni na chakula kikubwa ni pilau.

Wakati mwingine, naota ndoto kwamba ninaswali, lakini nikiamka nakuta kuna vitendo nafanya kama vya kuswali. Najihisi kwamba hicho kitu nimekifanya ndotoni kabisa, na vitendo hivyo nikiamka naziendeleza.

Kwa wenye uelewa, naomba tujuzane.
 
Nyie watu wa jf haya mueleweshweje hamtaki kuelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…