Tickets zinakatwa station na bei inatofautiana kulingana na class husika, mfano first class hii mara nyingi inakua na bei ghali kidogo kutokana na service ambazo utakua unapewa kwenye treni.
first class hili ni behewa lenye watu wa 4 tu ina vitanda na meza, na socket ya umeme so kama una devices za kielectronic kama simu au laptop yako unaweza uka enjoy safari yako bila kuwa na hofu ya chaji na pia huduma ya msosi kwenye first class unapata
Second class sikumbuki idadi ya wasafiri kwenye hili behewa ila hii mara nyingi haina kitanda wala service ya bure hua unapewa meza tu, msosi unanunua kwa pesa yako, kitanda hamna so meza utatumia kuegama pindi usingizi ukikupata na gharama yake imepungua kulinganisha na first
third class hii ndio behewa lenye gharama nafuu zaidi halina meza wala stuli limewekwa viti tu ambavyo wanakaa wawili wawili, huku mara nyingi hakunaga idadi iliyo constant yya abiria, hili ndio behewa ambalo kunakua na abiria waliosimama baada ya kukosa siti. Ni behewa ambalo halifati itifaki, ni behewa ambalo halina mpangilio, ni behewa lenye makelele na uchafu mwingi