Naomba kuelimishwa ni kwanini Makamu wa Rais Samia hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli?

Acha dharau.muombe Mungu akupe hekima ndani ya moyo wako.
Hata hivyo, pamoja na katiba kumbeba ila walijua fika hana uwezo.... na ndo hiki tunachokiona leo.

Hivyo walijua kabisa ni garasa ndiyo maana ulitokea huo mzozo kabla ya kuamua kukubaliana na hiyo mnayoita katiba.

Je, umewahi kujiuliza kwanini hao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliomweka hapo wote aliwafurusha?
 
Kipi kibaya nilichoandika katika andiko langu?.mimi nimeombwa kuelimishwa.sasa badala ya kueleza wewe unaanza vitisho.wewe huwezi na hufai kuwa kiongozi kabisa.
Lucas Mimi Si chawa mwenzio,

Nimekushauri pima ulichokiandika kabla ya kupeleka public,

HOJA Yako unalazimisha watu waulize maswali ambayo majibu yake kamwe hayawezi kupatikana Kwa sababu maalum.

Pima uzito wa kinywa chako kabla hujaongea Lucas.
 
Sio mara ya kwanza na sio ajabu sheria kupindishwa na wala haitakuwa mwisho.

Boss ana moyo wa Upendo na wa kusamehe.

Hakuna faida yoyote inayopatikana kwenye Kisasi.

Madaraka Sio sababu ya kuumiza wengine.

Mwisho mchawi mpe mwanao akulelee.
 
Rais Samia Ni Akili kubwa,ni kiongozi mwenye maono,upeo na uzalendo wa hali ya juu sana. Ni kiongozi mchapa kazi sana na ndio maana hata jenerali Venance Mabeyo amempongeza kwa ulimi wake mwenyewe.
 
Lucas Mimi Si chawa mwenzio,

Nimekushauri pima ulichokiandika kabla ya kupeleka public,

HOJA Yako unalazimisha watu waulize maswali ambayo majibu yake kamwe hayawezi kupatikana Kwa sababu maalum.

Pima uzito wa kinywa chako kabla hujaongea Lucas.
Kama hoja imekuzidi kimo cha akili yako ni vyema na busara ukakaa kimya tu.
 
Naona una hoja 2 hapo
1: kwamba kuna uwezekano kuna hila zimefanyika

2: ni kwamba umedharau hivyo vyeo viwili vya waziri mkuu,mkuu wa majeshi na katibu mkuu kiongozi Basi nkujuze,

Kwa kuanza kukukumbusha ni kwamba katibu mkuu kiongozi ndio kiongozi wa shughuli zote za raisi plus yeye ndo kiongozi wa ulinzi na usalama ndani ya ikulu na hata ni kiongozi ndani ya TISS,

Hivyo katibu mkuu kiongozi anaplay part kubwa hasa kwenye swala la ulinzi na taarifa zote ambazo zinafanywa au ziko mezani kwa raisi mfano kuna kazi fulani ya 2B ambayo haikutangazwa kwa umma ambalo alipewa waziri fulani basi ni lazma KK kiongozi ahakikishe ameliweka sawa mostly kwenye situation kama hizi. Bila kusahau issue za ulinzi na usalama kwa kuhakikisha amesuka taarifa ya taratibu zote za ulinzi na usalama wakati wa msiba na maziko kwa ujumla.

Mkuu wa majeshi yeye ndo kiongozi mkuu wa maswala ya usalama ndani ya nchi yeye ndo mwenye kuhakikisha anazuia au kuvunja kila kiashiria cha uvunjifu wa amani au uhaini kipindi taarifa za kifo cha rais kinatangazwa/kutokea.

Naweza kusema hiki ndo kipindi ambacho jeshi linakuwa allert mno na masuala ya ulinzi hasa uhaini na hapa viongozi wengi wa juu wa jeshi wanakuwa under government surveilance kwa kujua au kutokujua maana nchi inakuwa haiko stable.

waziri mkuu huyu ndiyo mwenye kamati zote za maafa na misiba ya kitaifa na yeye ndo mratibu mkuu wa shughuli hizo habari za msiba ufanyike wapi nan ahudhurie na bajeti ya bei gani iandaliwe huyu ndiyo master minder

Mwisho na isiyo na muhimu ni makamu wa rais huyu yeye huandaliwa njia zote na hao watajwa hapo juu,kuhusu lini na muda gani apewe taarifa na lini aapishwe au kukabidhiwa nchi.

Sababu za kutokuambiwa kwa wakati hasa huwa ni kutotengeneza taharuki ndani ya nchi sababu rais wangu samia kama angeambiwa kuwa mwenzake amefariki sidhani kama angekuwa yule aliyekuwa ziarani vile na kumbuka wakati huo kulikuwa na fukuto la rais yuko wapi rais yuko wapi

Nimalizie kwa kusema kipindi kama hichi huwa ni kipindi kibaya mno kwa maropo ropo au wenye uchu wa madaraka kwani huwa ni kipindi cha lala salama jeshi linakuwa macho na ukiwa kimbele mbele au tishio ndug yangu tunakuaga
 
Wewe ni mzalendo lakini uchawa was kusifu hovyo hovyo umekufanya usielewe mambo makini makubwa ya nchi hii!!

Nakushauri sana Sana kuanzia leo ACHA kuandika nyuzi za kichawa chawa hazikusaidii;-

Sasa kada mwenzio nakusaidia kimawazo hapo chini;-

1.Kwanini mara baada ya kuapishwa Mama alimuondoa katibu mkuu kiongozi!!?na kumpa ubunge!!?ukijua kwanini utajua kwanini Mama yetu hakujua hayo!!!

2.Kwanini waziri wa ulinzi aliondolewa Kwa kutobadilishiwa wizara wa kipindi hicho!!?


3.kwanini Bado inadhaniwa alionewa huruma Kwa kupewa ubunge na mama huyo aliekua KK!!?

Ukitafuta majibu ya haya utajua kwanini mama yetu hakujua yale!!!

Mwamba de'levis namkubali sana Kwa code zake!!
 
Kulikuwa na kundi la wahuni waliotaka kupora madaraka kutokana na ujinga wao na tayari Wameshaondolewa kwenye system. Mabeyo aliona uwekano wa kuwa mhaini iwapo angekubaliana nao hivyo alikwepa mapema.
 
Noted

Tulimuaga mmoja!mwenzake akapewa ubunge Hadi Leo ni mkimya sana!!!nae kawekwa kiporo!!
 
Unasema makamu ye ndo apewe taarifa ni ujinga ye atafurahia kwamba atakuwa rahisi kwaiyo atokuwa aware so atulishwa inapotakikana ila atoana mabadiliko
 
We jamaa sidhani kama uko sawa upstairs au umekurupuka, wapi Hayati aliambiwa hawezi kupona? nenda kasikilize upya na uelewe, kama unasema umesikiliza na kuelewa na kuchambua na huu ndo uchambuzi wako basi unamatatizo.
Toka lini chawa akawa na uwezo wa kuchambua,yeye anachojua ni kusifia tu basi
 
Acha uongo
 
CCM imekula akili yote.
 
Je kuna miongozo ya utoaji taarifa?, kama ndiyo, ipoje? Yahani nani apewe kwanza, akifuatiwa na nani, mpaka wa mwisho.
 
Title yako inasema kupewa taarifa na si kutangaza ,mtu wa kwanza kupewa taarifa ni Janeth Magufuli yeye ndiye alikuwa Mkewe, mtu wake wa karibu sana kuliko hata huyo samia.
Nafikiri hapa ni vitu viwili tofauti. Kama rais wa nchi Janeth hahusiki na taarifa. Ila kama Magufuli angekuwa mume wa Janeth tu bila kuwa Rais taarifa ya kwanza ingemhusu. Ila pale Magufuli alikuwa anauguzwa na nchi, siyo mambo ya kifamilia yale
 
Je kuna miongozo ya utoaji taarifa?, kama ndiyo, ipoje? Yahani nani apewe kwanza, akifuatiwa na nani, mpaka wa mwisho.
Kwani katiba inasemaje juu ya mlolongo wa vyeo serikalini? Nani anafuata kiwadhifa akitoka Rais? Nani anatangaza kifo cha Rais kwa umma?
 
Nafikiri hapa ni vitu viwili tofauti. Kama rais wa nchi Janeth hahusiki na taarifa. Ila kama Magufuli angekuwa mume wa Janeth tu bila kuwa Rais taarifa ya kwanza ingemhusu. Ila pale Magufuli alikuwa anauguzwa na nchi, siyo mambo ya kifamilia yale
Hata usingemjibu huyo nyumbu maana inaonekana akili yake haipo sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…