Naomba kufahamishwa haya kuhusu Pikipiki

Naomba kufahamishwa haya kuhusu Pikipiki

Mkirua2

Member
Joined
Oct 15, 2019
Posts
30
Reaction score
30
Msaada jamani, HIVi pikipiki Kwa matumizi ya kawaida mtu anatakiwa afanyie service vitu gani na Kwa mda gani?

Pia boxer 150 mazuri yake na mabaya yake ni yapi

Kuna madhara ya kubana mafuta kwenye pikipiki

Unawezaje kutambua kifaa ulichofungiwa kama ni og kwenye pikipiki Hasa hizi za boxer

Pia kwann boxer vifaa vyake ni gharama sana
 
Oil, oil, badili kwa wakati kulingana na safari zako

Plug, carburator, air cleaner visafishwe mara kwa mara

Kwavile hizo boxer ni za wahindi basi vifaa vyake hakikisha ni made in india
 
zingatia ushauri wa mjumbe wa #

pia napanua maelezo tu

-boxer zinasharau mafundi, penda kumpa kazi fundi mwenye uzoefu nazo ma asiwe mbabaishaji hasa linapokuja hitaji la kuchokonoa injini na mfumo wa umeme

-oil ibadilishwe hata kabla ya km 1,000 zilizopendekezwa kutegemeana na mazingira unakoendeshea

-usinunue vipuri vya bei nafuu. fuata ushauri wa fundi unayemwamini. pia na onyo: usimwamini fundi ukampatia pesa akanunue kifaa agunge. nunua mwenyewe ma uhakikishe amekifunga kweli.

-boxer zina madeko, usipende kuwaazima azima vijana wasiojielewa waliozoea king lion, sinoray, houjue n.k wataoburuza na kukuachia skrepa
 
Back
Top Bottom