Naomba kufahamishwa kuhusu credit card na ina tofauti gani debit card?

Debt Card Haipo Tanzania
Debit card maana yake lazima uwe na hela kwenye akaunti ili uweze kufanya manunuzi. Ni hizi kadi ambazo wengi tunazo za mabenki tofauti,. Credit card ni ile inayokuwezesha kufanya manunuzi kwa mkopo halafu unaanza kulipa taratibu kwa interest. Uwezo wako wa kufanya manunuzi huwa una kiwango cha juu kutegemeana na kipato chako kinachoingia kwenye akaunti kwa mwezi au mwaka. Huduma zote hizi zipo Tanzania. mpaka kulipia huduma ya Uber au hata kubook Air BnB apartment au hoteli nchi yoyote duniani.
 
Jibu mujarabu.... muuliza swali na wengine waelewe tu kuwa, asilimia zaidi ya 80 wanaotumia kadi hapa tanzania ni debit cards... wengi wanaziita credit cards...
 
Ok ,kwa hiyo tofaut hapa ni kuwa credit card inanofanya online purchases sio lazima uwe na KIASI husika cha kitu unachonunua,ila debit card Ni lazima uwe na KIASI husika cha kitu unachonunua,?
 
Ok ,kwa hiyo tofaut hapa ni kuwa credit card inanofanya online purchases sio lazima uwe na KIASI husika cha kitu unachonunua,ila debit card Ni lazima uwe na KIASI husika cha kitu unachonunua,?
yes mkuuu. Na moja ya vitu vinavyowatesa middle class kwenye nchi zilizoendelea ni madeni ya credit cards
 
Jibu mujarabu.... muuliza swali na wengine waelewe tu kuwa, asilimia zaidi ya 80 wanaotumia kadi hapa tanzania ni debit cards... wengi wanaziita credit card
yes mkuuu. Na moja ya vitu vinavyowatesa middle class kwenye nchi zilizoendelea ni madeni ya credit cards
Asante sana kiongoz,na hii inshu ya PayPal vp hii ina uhusiano Gani na hizi debt & credit card
 
Asante sana kiongoz,na hii inshu ya PayPal vp hii ina uhusiano Gani na hizi debt & credit card
Paypal ni intermediary kwa maana badala ya kuexpose details za card yako kwa merchants au suppliers unatumia paypal kulipa. Lakini paypal ina information zako za card kwa hiyo inenda ku deduct hela kutoka kwenye card yako. Ni safer kuitumia. Maana kuna merchants wengine sio waaminifu kwa maana wanaweza kutumia details za card zako kufanya unauthorized transactions. Yaani wanakulipisha kitu ambacho hukununua. Na pia information za card yako zinaweza kuibiwa zikatumika kufanya manunuzi bila ya wewe kuidhinisha. Kwa kutumia paypal unapunguza risks
 
Asante sana kwa ufafanuz mzur mkuu,
 
Pia niksha verify ATM card yangu kufanya online purchases ndo tayar naweza kuitumia kama credit or debit card au kuna process za kufanya tofauti na Ku verify?
Nenda benki kawaambie unataka kufanya manunuzi online. Kama ni CRDB watakupa fomu ujaze. Kisha utaendelea na process za verification baada ya kutumiwa one time access code kwenye simu yako. Sijui utaratibu kwa NBC kama ni the same. Ni vyema ukafika kwenye tawi lolote la karibu nawe wakupe mchakato mzima
 
Ok thanks
 
ivi hii "M-PESA MasterCard" ni debt au credit card mana kuna sehem wananambia hawaitaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maana nyepesi Debit ni pesa yako katika AC yako ukitoa au kununua inatoka direct kutoka katika Ac yako, credit ni kama advance au loan wanaolipa ni Bank yako wewe unawalipa Bank yako baadae, kawaida ukilipa katika siku 40 hakuna interest kama ulitumia laki moja unarudisha laki moja automatic wanachukuwa katika AC yako, ukichelewa zaidi ya muda hapo kunakuwa na interest kidogo. na Credit card nyingi zinakuwa na limit kiasi gani unaweza kukopa. Unaweza kuwa umeweka limit laki moja hapo utakopa mpaka laki tu pesa ukirudisha card inajireset. Lugha ya mtaani ukiwa na laki moja mfukoni unaenda dukani unanunua vitu vya laki moja cash, credit ni kama unaenda dukani unachukuwa vitu vya laki moja malipo mwisho wa mwezi kwa dhamana ya Bakhresa hapo kakuwekea dhamana kama mfano tu, na unamwambia mwenye duka bill yangu ikifika laki ustitoe mpaka nilipe. Hiyo ndio tofauti kubwa. Sababu ya credit kukubaliwa kila sehemu ni sababu anayelipa ni Bank kwa hiyo uhakika zaidi ndio sababu ya credit card kuwa na nguvu kufanya malipo ya online au sehemu yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…