Kwa maana nyepesi Debit ni pesa yako katika AC yako ukitoa au kununua inatoka direct kutoka katika Ac yako, credit ni kama advance au loan wanaolipa ni Bank yako wewe unawalipa Bank yako baadae, kawaida ukilipa katika siku 40 hakuna interest kama ulitumia laki moja unarudisha laki moja automatic wanachukuwa katika AC yako, ukichelewa zaidi ya muda hapo kunakuwa na interest kidogo. na Credit card nyingi zinakuwa na limit kiasi gani unaweza kukopa. Unaweza kuwa umeweka limit laki moja hapo utakopa mpaka laki tu pesa ukirudisha card inajireset. Lugha ya mtaani ukiwa na laki moja mfukoni unaenda dukani unanunua vitu vya laki moja cash, credit ni kama unaenda dukani unachukuwa vitu vya laki moja malipo mwisho wa mwezi kwa dhamana ya Bakhresa hapo kakuwekea dhamana kama mfano tu, na unamwambia mwenye duka bill yangu ikifika laki ustitoe mpaka nilipe. Hiyo ndio tofauti kubwa. Sababu ya credit kukubaliwa kila sehemu ni sababu anayelipa ni Bank kwa hiyo uhakika zaidi ndio sababu ya credit card kuwa na nguvu kufanya malipo ya online au sehemu yoyote.