Naomba kufahamishwa kuhusu ugonjwa wa Gerd

Naomba kufahamishwa kuhusu ugonjwa wa Gerd

Pole sana kiongozi, ulifanikiwa kupata matibabu au bado tatizo linakusumbua?

Mimi nafahamu dawa za mimea, ukipenda naweza kukuandalia, nimeona na kuna mwingine pia ana tatizo la GASTRITIS.

Kiujumla Kwa yoyote mwenye tatizo la PEPTIC ULCERS, GERD, GASTRITIS dawa zake nazifahamu.

Naweza kumuandalia atakaependa. Utalipia tu 10,000Tshs kwa kuwa nitatumia muda na fedha kuandaa dawa hizo.

Aghalabu hiyo dawa utakayolipia 10,000Tshs huwa inatosheleza kwa matibabu mpaka kupona, mara chache kuhitajika dozi ya pili isipokuwa kwa tatizo lenye athari za muda mrefu.

Asanteni.
Nip tayar nipo mwanza
 
Nilikuwa na shida kama hyo nilitembea hospital kadhaa ikiwemo Rabinisia ila dawa hazikufua dafu.Nikapataa mzee mmoja nikaambiwa ana dawa za kienyeji till now nipo good.
huyo mzee yupo wp nipe namba zake
 
Pole,

GERD: Gastro Esophageal Reflux Disorder/Disease

Ni kitendo cha sehemu ya chakula iliyokwisha kuingia tumboni kurudi juu/sehemu ya juu ya njia ya chakula kabla ya tumbo.

Sababu ya msingi ya kitendo hiki ni kutokana na kulegea kwa kifundo kinachotakiwa kubana ili hali husika isitokee.

Kuna sababu mbalimbali zinazohusishwa kuwa chanzo:

1: Tatizo la kuzaliwa nalo

2: Henia kwenye tumbo

3: Unene uliopitiliza

4: Kupungua sana baada ya kuwa mnene

5: Presha kubwa ndani ya tumbo (ujauzito).

6: Matumizi ya baashi ya dawa

7: Nk.

Dalili
Dalili za tatizo husika huwa ni tofauti kulingana na hali husika

1: Kiungulia

2: Kikohozi cha mara kwa mara hasa siku

3: Kubanwa kifua

4: Mate machungu hasa asubuhi

5: Vidonda mdomoni

6: Kuwa na harufu mbaya mdomoni

7: Nk.

Tiba
Tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo kwa mhusika na kiaai cha tatizo:

1: Dawa

2: Mabadiliko kwenye mwenendo wa kimaisha

3: Upasuaji

A: Dawa
Dawa za kupunguza zaidi na kupanfilia mwenendo w chakula kwenye mfumo wa chakula paomja na kuondoa kichefuchefu hutumika.

B: Mgonjwa hushauriwa kuondoa visababishi alivyonavyo au vinavyoonekana kusababisha tatizo kwake.

1: Kutokutumia vyakula vyenye muwashawasha kama pilipili, tangawizi nk.

2: Kutokula vyakula vyenye mafuta mengi

3: Kutokula vyakula vichachu kama ndimu, limao nk.

4: Kutokula ukashiba sana

5: Kula saa tatu kabla ya kwenda kulala

6: Kuweka kitanda chako/ kuinua nyuzi 45 upande unaoweka kichwa.

7: Kuhakikisha unapata chakula kwa muda husika

8: Kuzingatia matumizi sahihi ya dawa husika

C: Upasuaji
Hufanyika kwa wale wenye henia kulingana na kiasi cha henia na pia wale wenye kiasi hatarishi zaisi cha ugonjwa kulingana na viwango.

NB: Kulingana na dalili husika wakati mwingine tatizo hili huusishwa na matatizo ya moyo au kifua hasa pumu, hivyo ni muhimu kwa mgonjwa kujieleza vyema na mtaalamu wa afya kuwa makini sana na wakati mwingine mi muhimu kuhuaisha vipimo zaidi kabla ya kutoa hitimisho.
Umeeleza vyema mkuu shukran
 
Back
Top Bottom