Naomba kufahamishwa kwa wanaojua ni changamoto gani imeikumba biashara ya samaki kutoka ziwa Victoria?

Chomo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2017
Posts
250
Reaction score
662
Salaam nyote, poleni na mihangaiko ya utafutaji.

Wakuu mm ni mfanyabiashara wa kuuza samaki kutoka ziwa Victoria hawa sato na sangara, nikiri tu kwenye biashara hii ni mgeni yapata miezi 8 sasa.

Bei zimekuwa zikipaa kila leo bila kushuka imepelekea walaji kupunguza manunuzi na hivyo biashara kuwa ngumu na isio na uhakika.

Naomba kujua shida ni nn kwa mlio wazoefu au mlio karibu na ziwani. Tetesi zinasema ziwa lilifungwa na halijafunguliwa bado, wengne wanasema serikali imeruhusu samaki kuuzwa sana nje ya nchi hivyo kumekuwa na uhaba kwa hapa ndani

Naomba kuwasilisha..
 
.Wavuvi wanavua kila siku kitu kinacho sababisha Samaki kupungua ziwani na bei kuongezeka maana demend ipo juu na supply ni ndogo
lakin nasikia ziwa lilifungwa kupisha kuzaliana tena,je ni kweli na halijafunguliwa bado?
 
Ni kweli limefungwa week imeisha nadhani karibuni litafunguliwa,bhuwa linafungwa kila baada ya week ili viumbe humo wazaliane wa kutosha
 
Sisi walaji tujifunze kula samaki wa kutoka maziwa mengine pamoja na mito. Na pia tujifunze kutumia samaki wa maji chumvi. Ukizoea Sangara na sato pekee unateseka sana.
 
Salaam nyote, poleni na mihangaiko ya utafutaji.

Wakuu mm ni mfanyabiashara wa kuuza samaki kutoka ziwa Victoria hawa sato na sangara, nikiri tu kwenye biashara hii ni mgeni yapata miezi 8 sasa.

Bei zimekuwa zikipaa kila leo bila kushuka imepelekea walaji kupunguza manunuzi na hivyo biashara kuwa ngumu na isio na uhakika.

Naomba kujua shida ni nn kwa mlio wazoefu au mlio karibu na ziwani. Tetesi zinasema ziwa lilifungwa na halijafunguliwa bado, wengne wanasema serikali imeruhusu samaki kuuzwa sana nje ya nchi hivyo kumekuwa na uhaba kwa hapa ndani

Naomba kuwasilisha..
Hao samaki wewe unauzia maeneo gani? ili nikushauri jambo kidogo.
 
Npo mwanza,upatikanaj wa samaki umekuwa mgumu mno na uendeshaj wa kaz hz za uvuvi zimekuwa juu,pia wavuvi wamekuwa wajuaji sana wanauza lakin wew mnunuz unaweza usipate hata faida huko unakoenda kuuza

Ziwa bado halijafungwa
 
kwahyo tusitegemee mabadiliko ya bei siku za karibuni? kuna haja ya kubadilisha aina ya biashara sasa
 
Tena wakat huu wa mvua ndo ilitakiwa bei zishuke maana samaki hupatikana kwa wingi,ukiona mpaka mwez wa tatu mambo yabadiliki usitegemee tena kuwa yatakuwa sawa
 
Majeshi yanayozunguka ziwa Victoria wafungue vitaru vya kuzarisha miche ya samaki namaanisha samaki wazalishww sehemu maalumu badae warudishwe ziwa Victoria katika mazingira ya asili.
 
Kwann usijaribu kuuza sato za kutoka ziwa tanganyika na migebuka mimi nafanya io kazi pia
 
Back
Top Bottom