Naomba kufahamishwa mambo haya kuhusu kilimo cha Numbu

Unknown1

Member
Joined
Mar 9, 2021
Posts
70
Reaction score
45
Wapwa kwema?

Wakuu, naomba tupeane taarifa yoyote inayohusu hiki kilimo (niko interested nacho);

Mfano:

Wapi kinalimwa kwa wingi,
Mtaji wa kuanzia
Eneo lipi zuri la kulima
Eneo la kuanzia (ukubwa)
Soko lake linaweza kua wapi na zingine zote unazozijua wewe!

Karibuni wapwa, tujenge safari ya matumaini.
 
Katikati ya kigoma na kasulu nilikuaga naziona, jaribu kufatilia huko
 
Njombe zinapatiakana kwa wingi, ukiweza pata mawasiliano na watu wa huko.
 
Mtazamo wangu unaona; Unatafuta taarifa za kilimo kisicho na Tija... Kwa jinsi numbu zinavyolimwa hazihitaji ukisasa kwa maeneo nilikoshuhudia wakilima. Zinalimwa sehemu kame aridhi yenye asili ya mbuga. Yaani hazitaki sehemu yenye rutuba kwa mujibu wa walaji
 
Ofcoz yes! maana pia nliuliza kuhusu hichi kilimo, taarifa nlizozipt ni nyingi pamoja na hzi ulizosema !!! unajua kuna sku nlienda kijijin nlikutana na mtu alielima numbu! so I was so excited if I could take an opportunity unfortunately kilimo chenyewe ndo hicho!

Thanks for knowledge bruhπŸ™
 
Natumae mleta mada umepata muongozo...
 
Numbu ni nini? Au kuna Jina lingine maarufu?
 
Zinalimwa sana Njombe hata Mbeya pia ila nadhani hazina ishu kiuchumi. Labda kama umeshachungulia soko. Nimecheka kuna mtu kauliza Numbu ni nini nikakumbuka ukitamka Numbu Usukumani wanatambua ni Viazi vitamu. N wayz zenyewe hizi hapa![emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ (kuhus alieulz numbu ni nin) ..Asante saana mkuu kwa hiliπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Numbu ni nini? Au kuna Jina lingine maarufu?
Ni aina fulani hivi jamii ya viazi vitamu Ila vyenyewe haviwi vinene na vinalimwa Sana nyanda za juu kusini na hazina Radha yoyote
Pia ni vizuri kwa kuliwa na wagonjwa na ukiona mgonjwa wako kakataa kula nunbu uyo subilini kuzika tu
 
Ni aina fulani hivi jamii ya viazi vitamu Ila vyenyewe haviwi vinene na vinalimwa Sana nyanda za juu kusini na hazina Radha yoyote
Pia ni vizuri kwa kuliwa na wagonjwa na ukiona mgonjwa wako kakataa kula nunbu uyo subilini kuzika tu
HAhahaha!! afu hii inaeza kua fursa ujue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…