Naomba kufahamishwa Shule ya Msingi ya Kikristo iliyopo Goba, Mbezi, Madale, Kunduchi au Mbezi Beach

Naomba kufahamishwa Shule ya Msingi ya Kikristo iliyopo Goba, Mbezi, Madale, Kunduchi au Mbezi Beach

mzeemzima

Senior Member
Joined
Apr 14, 2010
Posts
123
Reaction score
78
Wadau,

Kwa unyenyekevu naomba kufahamishwa kwa mtu yeyote anayejua shule yoyote ya msingi ya Kikristo iliyoko katika maeneo ya Goba, Mbezi au Madale, Kunduchi, au Mbezi Beach. Kama unafahamu shule ya namna hii iliyoko eneo lolote jingine Dar es Salaam. Naomba pia kufahamishwa ingawa kipaumbele ni maeneo niliyoyataja.

Ninaposema shule ya Kikristo namaanisha shule ambayo inaweka msisitizo kwa watoto kujifunza masomo ya kawaida lakini pia na neno la Mungu, ikiweka msingi kuwa mtoto anahitaji kulelewa katika maadili ya kibiblia na kufundishwa kulishika na kuliishi neno la Mungu. Kipaumbele ni shule ambazo zinafuata mfumo wa Tanzania wa NECTA, lakini kama zipi zinzofuata mfumo au mtaala wowote mwingine itakuwa vema pia kuzifahamu.

Wenzetu Kenya wana shule kama hizi hapa chini, itakuwa vema kufahamu kama kuna shule za namna hii hapa kwetu Tanzania.

Thika Road Christian School , Curriculum

Jabali Christian Schools , Home


Natanguliza Shukrani
 
Asante wadau , kama kuna yeyote anayeifahamu nyingine zaidi ya Liebermann , naomba utushirikishe pia.
 
Lengo lako ni lipi? Tuorodheshe tu Shule basi!
 
Back
Top Bottom