Naomba kufahamishwa taratibu za kuanzisha chama cha siasa?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
1. Je, kuna hatua ngapi katika kusajili chama?

Ndio, kuna hatua mbili. Usajili wa muda na usajili wa kudumu.

2. Je, ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa muda?

• Wanzilishi wawili watawasilisha maombi ya usajili wa muda kwa kujaza fomu maalumu wakiambatanisha na katiba na kanuni za chama kitarajiwa. • Chama tarajiwa kinatakiwa kutoa uhuru wa mtanzania yoyote kuweza kujiunga bila kuwa na ubaguzi wowote wa kijinsia,kidini, kiitikadi n.k • Kulipa ada ya maombi ya usajili ya shilingi 25,000. Usajili wa muda utadumu kwa muda wa siku 180, ndani ya muda huo, chama kitatakiwa kutafuta wanachama wasiopungua 2000 ( 200 kwa kila mkoa) katika mikoa 10, mikoa miwili kati ya hiyo ni lazima iwe Tanzania Zanzibar na mkoa mmoja kati ya hiyo miwili, uwe Pemba. Kutimiza masharti ya usajili wa muda yaliyopo kwenye sheria

3. Je, ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa kudumu?

• Baada ya kupata wanachama 2000 ndani ya siku 180, Waanzilishi watawasilisha maombi ya usajili wa kudumu kwa kujaza fomu maalumu. Kulipa ada ya usajili wa kudumu ya shilingi 50,000. Chama kiwe kimepata Ofisi ya Makao makuu na anuani ya posta kwa ajili ya mawasiliano rasmi na kuchagua viongozi wa kitaifa. Chama kiwe kimetimiza masharti yote ya kupata usajili wa kudumu yaliyopo kwenye sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho 2015.
 
Tutaanzisha chama cha kidemokrasia kitakachokuja kumenyana vilivyo na CCM.Hizi takataka saccos za watu Chadema, Act wazalendo, Nccr mageuzi,Cuf,Udp n.k vimejaa ujinga ujinga
 
Wakuu salaam,

Baada ya kulazimishwa na JF kuwa napata "threads" kutoka Jukwaa la Siasa, hiki ndicho nilichoamua kufanya.

Nimeamua nami nianze harakati za kiungia kwenye list ya movers and shakers wa siasa ucharwa za bongo.

Baada ya kusema hayo naomba kujua ama kupatiwa vigezo stahili na vya msingi ambavo vinaitajika ilichama cha siasi kiweze kisajiliwa na msajili - Tanzania Bara.

Asante kwa wakati wako.

Cc Msajili
 
1. Je kuna hatua ngapi katika kusajili chama?

Ndio, kuna hatua mbili. Usajili wa muda na usajili wa kudumu.

2. Je ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa muda?

• Wanzilishi wawili watawasilisha maombi ya usajili wa muda kwa kujaza fomu maalumu wakiambatanisha na katiba na kanuni za chama kitarajiwa. • Chama tarajiwa kinatakiwa kutoa uhuru wa mtanzania yoyote kuweza kujiunga bila kuwa na ubaguzi wowote wa kijinsia,kidini, kiitikadi n.k • Kulipa ada ya maombi ya usajili ya shilingi 25,000. Usajili wa muda utadumu kwa muda wa siku 180, ndani ya muda huo, chama kitatakiwa kutafuta wanachama wasiopungua 2000 ( 200 kwa kila mkoa) katika mikoa 10, mikoa miwili kati ya hiyo ni lazima iwe Tanzania Zanzibar na mkoa mmoja kati ya hiyo miwili, uwe Pemba. Kutimiza masharti ya usajili wa muda yaliyopo kwenye sheria

3. Je ni nini kinahitajika ili kupata usajili wa kudumu?

• Baada ya kupata wanachama 2000 ndani ya siku 180, Waanzilishi watawasilisha maombi ya usajili wa kudumu kwa kujaza fomu maalumu. Kulipa ada ya usajili wa kudumu ya shilingi 50,000. Chama kiwe kimepata Ofisi ya Makao makuu na anuani ya posta kwa ajili ya mawasiliano rasmi na kuchagua viongozi wa kitaifa. Chama kiwe kimetimiza masharti yote ya kupata usajili wa kudumu yaliyopo kwenye sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho 2015.
Ongea na CCM mradi uwe tayari kuipopoa Chadema kesho usajili utakamilika.
 
Back
Top Bottom