Naomba kufahamishwa taratibu za kupata Hati Miliki ya Nyumba

Naomba kufahamishwa taratibu za kupata Hati Miliki ya Nyumba

Wababa13

Senior Member
Joined
Dec 27, 2017
Posts
105
Reaction score
70
Wana-Jukwaa habari ya muda huu, naomba kufundishwa jinsi ya kupata hati miliki ya nyumba, baada ya kuandikishana kwenye kitongoji husika sasa nahitaji kupata Hati Miliki
Natanguliza shukurani.
 
Sijawahi kusikia hati miliki ya nyumba, uwa nasikia hati ya ardhi ambayo mchakato wake unafanyika halmahauri, fika huko onana na idara ya Ardhi watakusaidia.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Sijawahi kusikia hati miliki ya nyumba, uwa nasikia hati ya ardhi ambayo mchakato wake unafanyika halmahauri, fika huko onana na idara ya Ardhi watakusaidia.
Asante sana 🤝🏾
 
Wana-Jukwaa habari ya muda huu, naomba kufundishwa jinsi ya kupata hati miliki ya nyumba, baada ya kuandikishana kwenye kitongoji husika sasa nahitaji kupata Hati Miliki
Natanguliza shukurani.
Fika serikali yako ya mtaa watakupatia utaratibu wote
 
Kwa utaratibu zilizowekwa kuzingatiwa vinginevyo utaanza uoya......
Kama ni.....
1. Nyumba ni ya Urithi ambayo imefunguliwa Mirathi basi mikataba ya mauziano iliyofanyika Kwa Mwanasheria anayetambulika,oamoja na Hati ya usimamizi wa Mirathi ambaye naye atakupa form ya kukutambulisha kuwa wewe ndiye mmiliki wa sasa ambapo Halmashauri au ardhi utawalipa gharama za Uhamisho wa umiliki na gharama zingine
2. Kama anayekuuzia Nyumba ni Mmiliki basi ni vizurikuuziana mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri husika au Ardhi kwani hii itakuepusha kulipa mara mbili......Kisheria Mwenuekiti au Mtendaji wa Kijiji, Mtaa hawaruhusiwi kusimamia uuzaji wa Nyumba......wanadai 10% ambayo inaishia matumboni mwao na Haina risiti.......
3. Ni vizuri kupata taarifa ya Eneo husika kabla hujanunua Ili kujua watu wa Ardhi kwenye Mipango miji wametenga Kwa ajili ya nini?
4.Maelekezo yapo mengi Tafuta Mwanasheria akuelekeze nini Cha kufanya
 
Back
Top Bottom