Mfano:kodi ya frem 150, 000 kwa mwezi, kodi ya zuio ni 150, 000*10% utapata 15000 kwa mwezi. Unatakiwa ulipe ya mwaka mzima kwa hiyo 15000*12=180, 000 jumlisha stamp 18000/= so utatakiwa kulipia 198, 000/= kisha anakukadiria kodi yako sasa utakayotakiwa kuilipa kutokana na maelezo uliyompa kuhusu biashara yako, mfano una mtaji kiasi gani pamoja na hiyo kodi uliyolipa kwa muda gani ili aangaliye mtaji wako kisha akukadirie. Mfano ktk from kuna kipengele cha mtaji uliowekeza na mapato utakayoingiza kwa mwaka.. Hapo ndiyo sehemu anayotumia kukuchinjia... Mfano anaweza akakukadiria kodi ya mwaka 300, 000 kwa kuanzia atagawanya mara 4 =75000/= ambayo utatakiwa uilipe kila baada ya miezi mi3... Hivyo kwa kuanza ili upate leseni unatakiwa uwe na 75000+198, 000=273, 000/=jumlisha mhuri was mwanasheria 20, 000=293, 000/= hii ni mbali na leseni.. Hii ni TRA tuu... Bado manispaa
Soo TRA 293, 000 +LESEN MANISPAA 80, 000=373, 000/=