Hebu nikupe kidoogo version ya nyakusa history Yangu.
Miaka ya Mwisho ya 1600 na Mwanzo Kwa 1700 kulitokea njaa upogoroni, lakini njaa haikuwa eneo loote la upogoro Ni baadhi ya maeneo haswahaswa ya kondeni, yake ya kwenye miinuko na baadhi ya Konde nilikuwa na chukula bwerere. Lakini wengi WA wenye chakula walikuwa wachoyo! Sasa waliokosa chakula na kunyimwa wakaadhimia kuhama upogoroni, wakabembelezwa wakakataa I.e. Wakabisha, ndio asili ya neno(jina) wasokile yaani wabishi.
Hii Kwa version Yangu naiita Sokile migration, wasokile walivyoondoka walikuwa wanaacha wahanga njiani Kwa sababu kedekede, mfano wakafika upogoroni mabondeni wakawaacha wandamba na wabena, wakafika makete wakawaacha watu wote walioshindwa kuendelea na safari Kwa tatizo la kupasuka miguu(makegete) I.e ndio asili ya jina makette, wakaishia Suma then wengine wakapita njia mdefu wandali ili kufika Konde (Ngonde) a fertile land.