Naomba kufahamu huu ni ugonjwa gani

Naomba kufahamu huu ni ugonjwa gani

inaitwa Infectious coryza ni ugonjwa hatari wa bacteria ambao unaathiri mfumo wa upumuaji na huwa unaonekana kwa kuvimba macho na eneo chini ya jicho, kuku kutoa makamasi na kupiga chafya ugonjwa huu husababisha hasara kubwa.
cha kufanya
chukua wembe pasua huo uvimbe utatoa kitu cheupe kama gololi. weka dawa ya kidonda au paka ute wa jani la aloevera
safisha banda tumia dis infectant ya v-rid 20ml changanya na maji lita kumi na tano wape kuku vitamini kwenye maji,maana pia kupungua kwa vitamin A husababisha washikwe ugonjwa huo kirahisi. walishe majani kwa wingi na chakula kamili kutokana na umri wao. unaweza kutibiwa kwa kutumia antibiotic na dawa zenye salfa. uaweza kupata ushauri zaidi duka la dawa za mifugo

wafugaji wengi wanashindwa kutofautisha kati ya ugonjwa huu wa coryza na fowl pox (ndui)

fowl pox (ndui) wanakuwa na vidoti na madonda madonda mwili mzima mpaka hata baadhi ya sehemu za miguu na ukifunua mwanyoya na mabawa utaviona
coryza ni kama inavyoonekana kwenye picha


https://web.facebook.com/makurainvestment/



upo sahihi mkuu,
 
Magonjwa ya kuku yanaumiza sana wafugaji wengi, mie pia nimepitia sana hizo changamoto pamoja na kutumia gharama kwenye madawa mara nyingine hazisaidii inakua kama bahati nasibu hasa pale ugonjwa unapokua ushawapata...
Kwa sasa nimeacha kabisa tumia madawa ya kununua, ni mwendo wa alovera, oregano na vitunguu swaumu tokea wanapoanguliwa na nashukuru tokea nimeanza hizi tiba mbadala huu ni mwaka na miezi 2 kuku hawajawahi kufa wala kushambuliwa na ugonjwa hatarishi...
Oregeno ndo nini mkuu? Naje unachanganya?au kila dawa kwa wakati wake? Na unawapa kila baada ya muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sikosei wanasema ni corayza
Na kuna dawa ya kuwawekea kwenye maji wanywe
Pia unatakiwa umsafishe macho kwa pamba ambapo utatakiwa kumtoa huo uchafu huko machoni ambao unakuwa utando mweupe ukisha msafisha ndipo unamwekea hiyo dawa kwenye macho
Kwa uzoefu wangu, hii ni corayza ambayo chanzo chake ni mafua. Wape Dawa inatwa tyrodox au tyrofarm. Hao waliovimba macho, chemsha maji yawe ya vuguvugu, weka chumvi kidogo sana. Chukua pamba wasafishe macho,huwa unataka uchafu mweupe,kama huna Dawa ya kuwapaka wapake mafuta ya Nazi au ya kula kwenye kingo za macho zinazokutana wakati wa kufumba. Kupoa kunachangiwa na kutokula pia,hivyo hakikisha unawalisha na kuwanywesha Dawa nilizoandika hapa. Unatakiwa kuwa Karibu nao sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dudupori, umeweka vitu vitatu hapo, kwenye maelezo yako arovera, vitunguu swaumu na kingine hicho in nini?

Oregeno ndo nini mkuu? Naje unachanganya?au kila dawa kwa wakati wake? Na unawapa kila baada ya muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmea wa oregano upo maeneo mengi ila wengi wanaufahamu kwa majina tofauti...
20190105_131521-1.jpeg
 
Oregeno ndo nini mkuu? Naje unachanganya?au kila dawa kwa wakati wake? Na unawapa kila baada ya muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa nachuma majani hayo ya oregano kiasi cha mkono mmoja, jani moja la alovera lililokomaa vizuri na unene wa kutosha na kitunguu swaumu kimoja kikubwa, navitwanga vyote kwa pamoja hadi vilainike vizuri then naloweka na maji kiasi cha lita moja na nusu hadi mbili kutegemea na mchanganyiko wako ulivyo kwa muda usiopungua masaa sita. Baada ya hapo nachuja vizuri na kuweka kwenye chupa safi na kuhifadhi kwa jokofu ili usichache haraka na naweza kuutumia hata kwa wiki mbili, ikiwa huna jokofu ni vyema mchanganyiko wako uuchemshe kidogo kwa dk 10 ili kuzuia kuharibika mapema...
Sasa kwenye matumizi yake unachukua kiasi cha robo kikombe na kuchanganya na maji lita moja ndo unawapa kuku wako kwa siku tata mfululizo na waweza rudia hivyo kila mwezi ili kuwapa kuku wako kinga zaidi...
Tahadhari hii tiba yangu haijathibitishwa kisayansi ila kwa upande wangu naweza sema imenisaidia sana kwani nina zaidi ya mwaka na nusu sijanunua dawa yoyote ya kisasa, kikubwa zaidi msisahau kuwapa chakula chenye mchanganyiko mzuri kwa afya bora...
 
Back
Top Bottom