Naomba kufahamu huu ni ugonjwa gani




upo sahihi mkuu,
 
Oregeno ndo nini mkuu? Naje unachanganya?au kila dawa kwa wakati wake? Na unawapa kila baada ya muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sikosei wanasema ni corayza
Na kuna dawa ya kuwawekea kwenye maji wanywe
Pia unatakiwa umsafishe macho kwa pamba ambapo utatakiwa kumtoa huo uchafu huko machoni ambao unakuwa utando mweupe ukisha msafisha ndipo unamwekea hiyo dawa kwenye macho
Kwa uzoefu wangu, hii ni corayza ambayo chanzo chake ni mafua. Wape Dawa inatwa tyrodox au tyrofarm. Hao waliovimba macho, chemsha maji yawe ya vuguvugu, weka chumvi kidogo sana. Chukua pamba wasafishe macho,huwa unataka uchafu mweupe,kama huna Dawa ya kuwapaka wapake mafuta ya Nazi au ya kula kwenye kingo za macho zinazokutana wakati wa kufumba. Kupoa kunachangiwa na kutokula pia,hivyo hakikisha unawalisha na kuwanywesha Dawa nilizoandika hapa. Unatakiwa kuwa Karibu nao sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oregeno ndo nini mkuu? Naje unachanganya?au kila dawa kwa wakati wake? Na unawapa kila baada ya muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa nachuma majani hayo ya oregano kiasi cha mkono mmoja, jani moja la alovera lililokomaa vizuri na unene wa kutosha na kitunguu swaumu kimoja kikubwa, navitwanga vyote kwa pamoja hadi vilainike vizuri then naloweka na maji kiasi cha lita moja na nusu hadi mbili kutegemea na mchanganyiko wako ulivyo kwa muda usiopungua masaa sita. Baada ya hapo nachuja vizuri na kuweka kwenye chupa safi na kuhifadhi kwa jokofu ili usichache haraka na naweza kuutumia hata kwa wiki mbili, ikiwa huna jokofu ni vyema mchanganyiko wako uuchemshe kidogo kwa dk 10 ili kuzuia kuharibika mapema...
Sasa kwenye matumizi yake unachukua kiasi cha robo kikombe na kuchanganya na maji lita moja ndo unawapa kuku wako kwa siku tata mfululizo na waweza rudia hivyo kila mwezi ili kuwapa kuku wako kinga zaidi...
Tahadhari hii tiba yangu haijathibitishwa kisayansi ila kwa upande wangu naweza sema imenisaidia sana kwani nina zaidi ya mwaka na nusu sijanunua dawa yoyote ya kisasa, kikubwa zaidi msisahau kuwapa chakula chenye mchanganyiko mzuri kwa afya bora...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…