Naomba kufahamu kisimbusi kitakachoonesha Euro 2016 mbali na DSTV

Bia batta

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
66
Reaction score
34
Hv washika dau ukiacha "beberu" Dii Esi Tii Vii na chanel zake za SS, hakuna kisimbusi chochote local and affordable kitakachoonyesha hii michuano ili tufanye mchakato tukilipie hata leo ili tuangalizie haya mashindano tukiwa makwetu badala ya kujazana kwenye ma-bar na vibanda umiza kuziangalia timu zetu pendwa.

Hawa makaburu ada za vifurushi vyao ziko juu sana asee kiasi kwamba kama ni mtu wa kipato cha kawaida ukiamua kulipia unaweza sababisha watu wasipate mahitaji muhimu nyumbani......!!

Kama kuna yeyote mwenye taarifa za uhakika embu tujuzane.
 
Ngoja waje bt jiandae maana majibu mengine yatakua hayaendani na mada@
 
Hivi vyote ni hamna kitu wadau tushasema kitambo zipo alternative powervu ni mambo yote kuanzia epl,uefa,bundesliga,laliga,ueuro,movies etc pasipo malipo yoyote
Hii ikoje, embu tupe maujuzi....nafahamu kuna online TV na ile live soccer TV ya simu but mara nyingi mtandao huwa ni changamoto as mawimbi hayawi clear inayopelekea picha kunasanasa...!!
 
AZAM TV Wameshatoa matangazo juu kurusha LIVE EURO kupitia Chanel ya ZBC2 ni sahihi naonaga mwenyewe matangazo yao kila siku kwenye tv ya Azam.
 
Azam wanazingua sana,pia kwanini Dstv tulipie kwa dolla,inatuumiza sana sana
 
Okay, but kuhusiana na AZAM TV nimejaribu kufuatilia kwa kupiga ile number yao (0764-700 222) kuna dada mmoja wa customer care ananiambia hata yeye hana uhakika kuhusiana na kurushwa live kwa haya mashindano but taratibu zinafanyika nafkiri hadi june mwanzoni ndo watakuwa na uhakika.....kuhusiana na ZBC2 hata mimi nimeliona hilo tangazo ila wanachosema ni kuwa "WATAKUWA WANAFANYA UCHAMBUZI KUHUSIANA NA HAYA MASHINDANO KABLA HAYAJAANZA RASMI" yaani ile wanaita road to france, but nafkiri nitakuwa makini kwenye kusikiliza hilo tangazo litakaporuka tena.
 
Kwa DSTV ni kifurushi gani kitakuwa kinaonyesha na inalipiwa kwa Shilingi ngapi?
 
hiyo tv yako ipo tofauti na yangu, kwangu tangazo lipo very clear kuwa ZBC2 LIVE UERO 2016!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…