Naomba kufahamu kuhusu 2006 Suzuki Escudo 2.7xs

Naomba kufahamu kuhusu 2006 Suzuki Escudo 2.7xs

Usishtuke mkuu sio bei hiyo. Ni gari inahitaji matunzo. Service lazima ufanye kwa usahihi na kuweka vimiminika sahihi. Sio oil za arusha njiro. Engine naWeka total quatz 5w 30 Gear box unaweka transmission fluid T-IV ya toyota. Na huwa sibadili vimiminika. Air filter badili kila service 2. Au hakikisha ni safi kila wakati. Inatumia sana upepo. Mashine ni kiboko Hazisumbui kwa maana ya kuharibika hovyo. Pata ambayo ni 4wd. Suspension iko Sawa sana. Kwa safari ndefu ni nzuri sana. Ina nafasi ya kutosha sana ndani buti kubwa ya kuweka mizigo. Ac yake iko njema sana. Sio zile za kujaza jaza gesi. Ikiwa unamatumizi makubwa na upo mjini unaweza ku combine na Gesi asilia sehemu kuweka mitungi ni ya kutosha.
Okay shukrani mkuu.
 
Back
Top Bottom