Naomba kufahamu kuhusu ARV

Naomba kufahamu kuhusu ARV

Nduka Original

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,012
Reaction score
817
Naomba kufahamishwa kwamba ni kweli mgonjwa akisha anza kutumia ARV hawezi kuambukiza ugonjwa?? Kuna jamaa hapa mtaani kaathirika ila anatumia ARV kwa muda na ukimuona afya yake iko imara. Shida huyu jamaa anatembea na watoto wadogo wadogo ila nasikia kwamba sababu anatumia ARV basi hawezi kuambukiza? Je hili ni kweli?
 
Kama anatumia ARV vizuri viral load yake itakuwa ipo chini na ni kweli uwezekano wa kuambukiza unaondoka kwa asilimia nyingi..ndo maana watu wanahimizwa kutumia ARV vizuri.

Lakini hili pia halihalalishi jamaa kugegeda hao watoto mtaani kiholelea kama anavyofanya
 
Punguza hofu nduka Kama umesex nae, kapime rudia kupima tena miezi mitatu baada ya tendo uwezekano wa kukuambukiza ni mdogo sana japo nae anaweza kukuambukiza tahadhali muhim
 
Naomba kufahamishwa kwamba ni kweli mgonjwa akisha anza kutumia ARV hawezi kuambukiza ugonjwa?? Kuna jamaa hapa mtaani kaathirika ila anatumia ARV kwa muda na ukimuona afya yake iko imara. Shida huyu jamaa anatembea na watoto wadogo wadogo ila nasikia kwamba sababu anatumia ARV basi hawezi kuambukiza? Je hili ni kweli?
Mgonjwa akitumia ARV kuanzia miezi mitatu inasemekana Hawezi tena kuambukiza kwenda kwa mwingine na hii inatokana na ARV kufubaza Virusu vya Ukimwi(VVU) na ndio Maana Cd4(Kinga ya Mwili) inaonekana Kupanda Over.
 
Nasikia ni kweli,kwa 98% vidoge hivyo Nika ilivyo vidonge vya Tb ukianza tu kutumia hawez ambukiza mtu
 
Naomba kufahamishwa kwamba ni kweli mgonjwa akisha anza kutumia ARV hawezi kuambukiza ugonjwa?? Kuna jamaa hapa mtaani kaathirika ila anatumia ARV kwa muda na ukimuona afya yake iko imara. Shida huyu jamaa anatembea na watoto wadogo wadogo ila nasikia kwamba sababu anatumia ARV basi hawezi kuambukiza? Je hili ni kweli?
Kama umefanya mapenzi na mzee wa kifurushi cha maisha pasipo kutumia kinga nenda tu na wewe kajiunge na kifurushi cha maisha.
 
Hivi hakuna sheria za kuwabana watu wanaotumia mbaazi kuambikiza watoto wadogo ukimwi kimakusudi?
 
Kama anatumia ARV vizuri viral load yake itakuwa ipo chini na ni kweli uwezekano wa kuambukiza unaondoka kwa asilimia nyingi..ndo maana watu wanahimizwa kutumia ARV vizuri.

Lakini hili pia halihalalishi jamaa kugegeda hao watoto mtaani kiholelea kama anavyofanya

Naam!
Viral load ikiwa chini (tena ifike mahali iwe hata below 50 ISiwe detected) inapunguza risk ya ya kuambukiza!

Ila inashauriwa kutokua na tabia hatarishi maana hao anaotembea nao (assume bila kinga) afya yao ikoje, ni very risk mwenye virusi akipata aina ingine tena na ya maambukizi.

Ndio maana inashauriwa kuzingatia tiba ila kuishi RESPONSIBLE SEXUAL LIFE STYLE!
 
Hivi hakuna sheria za kuwabana watu wanaotumia mbaazi kuambikiza watoto wadogo ukimwi kimakusudi?

Kwa uswahili wetu sidhani kama iko very straight maana wafanya maamuzi wetu huwa wanakwepa sheria ambazo zinaweza kuwa chungu! Ila ni issue very sensitive Mkuu.
 
Mnajazana ujinga lakini siku ukiupata utaumia mwenyewe na sio na hawa wanao-comment
 
UONGOOO Kutumia dawa za ukimwi hakukufanyi usiwez na uwezo wa kuambukiza wengine kabisa... Ila ukitumia dawa hizi vizuri na kwa muda mrefu husaidia kupunguza Viral Load ifike almost Undetected kwamba Virus vimefubazwaa kiasi kwamba ni kama havipo kwenye damu tenaa.. mtu akifika stage hii hawezi kuambukiza mtu na pia hata Ukimpima kwa zile Rapid test ya HIV Itaoneshaa Negative. Kufika hatua hii sio jambo la siku moja wala sio rahisi inafaa uzingatie matumizi mazuri ya dawa na mloo mzuri.
 
Back
Top Bottom