Naomba kufahamu kuhusu mishahara ya walimu

Naomba kufahamu kuhusu mishahara ya walimu

Jaman naomba kufahamishwa kwa wale ambao wapo kwenye sekta ya elimu (walimu)kwa sasa mishara kwa level ya cheti, stashada na shahada ni kiasi gani kwa maana mm pia najiaanda kuwa mwalim.

kwakua unataka kuwa mwalimu na umeshapata data juu wa udogo wa mshahara, basi unatakiwa kujipanga ili usizeeke ukiwa na hali mbaya.
Fahamu ya kwamba, hata secta zetu (secta nyingine) ni siri yao tu. Hata kwetu hali sio nzuri. Ila kwa uchache watu, ndio maana kilio chatu hakina sauti kama cha walimu.

Pengine tunafanya kazi chini ya sheria kali na adhabu ya kupata ajira ikiwa tutatimulia mahali tulipo, ndio sababu ya kuishi kama mabubu.
Kwa kua uko katika utafutaji, basi kufanya kazi zaidi ya moja ni bora zaidi! Ndio maana hata viongozi wa nchi yetu wana vyeo lukuki, wakati huo huo wakifanya biashara mbalimbali.

Vyeo lukuki haina maana kua watu wa kushika nafasi hawapo, bali inamaana kua wao wako katika utafutaji.
Kazi zaidi ya moja ndio mkombozi wa kila mtu!
 
ENANTIOMER,

Ushauri mzuri sana.... Mimeupenda.
 
Last edited by a moderator:
Ajira za umma ni zaidi ya mshahara.kuna wakati tunafanya kazi bila faida binafsi kwa masilahi ya wasio na uwezo wa kufanya kazi pamoja na kuongeza thamani na faida ya utu wetu kwa watu wengine wanaohitaji huduma.

mfano.kazi ya mwalimu ni kuelimisha jamii.,mwalimu anaejitambua kazi kwake ni zaidi ya mshahara;halikadhalika dakitari,mwanasheria,injinia,afisa mtendaji wa kijiji,mbunge,waziri,na raisi.

Tukiwa na mtazamo wa kuhudumiana kuliko kunyonyana kila mtu atafaidi matunda ya kazi yake na hakuna kazi itaonekana ni bora kuliko nyingine kwani kazi zote zinategemeana katika kutoa huduma kwa mwanadamu wa leo na kesho.

Lakini tukiendelea na mtazamo finyu wa kutengeneza pesa na kupiga madili bila kujali utu wa watu wengine matokeo yake ni mmomonyoko wa maadili,ufisadi (kila mtu anawaza dili-ESCROW),ujambazi,kufanya kazi chini ya kiwango,utegemezi wa fikra na kipato hatimae umaskini uliokithiri.

Niwajibu wa kila mtu kufanya kazi kwa malengo ya kuibadili dunia yake na dunia ya watu wengine,tusiweke sana maslahi binafsi mbele!!!Ila tujiulize dunia itatukumbuka kwa lipi baada ya sisi kuondoka.....ni kazi pekee itakayokupa frusa ya kukumbukwa katika zuri au baya...iwe binafsi ama ta umma.

"If you don't like something change it,if you can't change it...change your attitude"

Maya Angelou !
 
TH inategemeana na makato mf.ukijiunga na NSSF 10%,LAPF-GEPF-PSPF-PPF 5%,CWT 2%,NHIF 3%,Then PAYE---
wapo wanaopokea 510000= wengine 474000/=
 
NI MAWAZO YANGU, inawezekana muuliza swali hata hasomei ualimu ni kejeli tu, kama ansomea ualimu then anauliza maslahi amepotea ualimu ni wito kama hana wito atafute kazi nyingine au aombe CCM iondoke madarakani labda mfumo ukibadilika maslah yataboreshwa.
 
Jaman naomba kufahamishwa kwa wale ambao wapo kwenye sekta ya elimu (walimu)kwa sasa mishara kwa level ya cheti,

Stashada na shahada ni kiasi gani kwa maana mm pia najiaanda kuwa mwalim.

Samahani ndugu hivi mwalimu anajiandaa au anaandaliwa??
 
Jaman naomba kufahamishwa kwa wale ambao wapo kwenye sekta ya elimu (walimu)kwa sasa mishara kwa level ya cheti, stashada na shahada ni kiasi gani kwa maana mm pia najiaanda kuwa mwalim.
200000
 
Hawajielewi huku chuo ni kutanua tu na hela za mikopo simu kali , pc bomba , kutokelezea kwa sana... Mshahara wenyewe ndo huo ! Kiruuuu ningekua mimi ningenunua bodaboda tu mapema mshahara ukiingiza ugali bodaboda iingize tembele.

Maana hako kaela na makato yote ayo ni kitanzi tu ! Education officer my foot poor officers.... !
 
Back
Top Bottom