Naomba kufahamu kuhusu RPL

Naomba kufahamu kuhusu RPL

Farmer82

Senior Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
183
Reaction score
39
Wadau wa elimu habari!

Samahani mimi ni Mtanzania niliepata elimu yangu ya form four mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kupata div 3 ya point 25, nikafanikiwa kuendelea na kidato cha tano, lakini kuna matatizo yalitokea ndani ya family, hivyo sikuweza kumaliza kidato cha sita.

Nikaingia mtaani kuhangaika na maisha miaka yote hiyo, na sasa nimedhamiria kurudi shule kufanya degree, tatizo ni kua natakiwa nifanye miaka mitatu kwanza (1 year certificate + 2 years diploma) ndio nianze bachelor, na mimi muda huo naona ni mrefu sana kwangu.

Nimesikia kua kuna test zinaitwa Recognation of Prior Learning (RPL) inatolewa na T.C.U na ukifaulu kwa kiwango fulani unakua eligible kusoma bachelor degree kwa universities za hapa nchini, kwa wale ndugu zangu wenye ufahamu wa jambo ili, au msaada mwingine wowote wa kiushauri naombeni mnisaidie.

Ahsanteni sana!
 
Mim nakushauri uwasiliane nao hao TCU ili wakupe majibu ya uhakika
 
Mim nakushauri uwasiliane nao hao TCU ili wakupe majibu ya uhakika

Ahsante mkuu,ila TCU nimewapigia simu sana lakini hawapokei!ndio maana nimeleta mada hapa kwa kua najua nitapata chochote!
 
wale watu wanafahulu wachache sana yani kama 5% ya wote walofanya mtihani shida sijafahamu ni nini ila waone tcu makao makuu utapata maelezo vizuri zaidi!
 
TCU wanatoa hiyo huduma ya program ya RPL toka 2013. Unachotakiwa ni kufanya registration kwa gharama ya Tshs 50,000/= kwa njia ya online www.cas.ac.tz na hiyo hela unalipa kwa njia ya mpesa akaunti namba 1234! Baada ya kufanya registration na kuchagua kozi uitakayo unasubiri kujulishwa siku ya kwenda kufanya mtihani ktk kituo utakachopangiwa. Kwa maelezo zaidi nitumie email address yako nikutumie tangazo lao.
 
Mkuu RPL walishafanya mitihani na wakatoa matokeo na kutaka waliofaulu kuomba vyuo nafikiri waweza kuwa umechelewa.japo kuwapigia mara kwa mara vema watapokea 2 cm
 
TCU wanatoa hiyo huduma ya program ya RPL toka 2013. Unachotakiwa ni kufanya registration kwa gharama ya Tshs 50,000/= kwa njia ya online CENTRAL ADMISSION SYSTEM na hiyo hela unalipa kwa njia ya mpesa akaunti namba 1234! Baada ya kufanya registration na kuchagua kozi uitakayo unasubiri kujulishwa siku ya kwenda kufanya mtihani ktk kituo utakachopangiwa. Kwa maelezo zaidi nitumie email address yako nikutumie tangazo lao.

Msaada kwa mtu mwenye division 4 ya 26 ya 2012 nae anaweza kupga msuli wa RPL?
 
Asante sana ndugu,nakuinbox email id yangu
 
Mkuu RPL walishafanya mitihani na wakatoa matokeo na kutaka waliofaulu kuomba vyuo nafikiri waweza kuwa umechelewa.japo kuwapigia mara kwa mara vema watapokea 2 cm

Asante ndugu,mimi najipanga kwa mwakani 2015,ila nilikua nataka kujua mapema utaratibu wa kujiregister na ufanyaji mitihani hiyo ukoje!Thanks again ndugu
 
Msaada kwa mtu mwenye division 4 ya 26 ya 2012 nae anaweza kupga msuli wa RPL?

Mpaka mtu wa darasa la saba anaweza fanya mkuu,ila wanasema unatakiwa uwe na experience ya kile unachotaka kwenda kusomea,hapo ndio sielewi,maana kama mimi nataka nikasome business admin,na sijawahi kuajiriwa,nafanya biashara zangu za kuunga unga tu wala haziko registered!
 
Back
Top Bottom