Naomba kufahamu lishe ya mtoto

Naomba kufahamu lishe ya mtoto

Nilisoma mahali kwenye group fulani kuwa kuchanganya aina mbalimbali za lishe na kuipika kwa pamoja haileti maana iliyokusudiwa, I mean karanga, wheat etc yaani kila kitu kipikwe kivyake

Sasa mimi nawawekea tofauti tofauti yani ulezi yenyewe, unga yenyewe, nafaka za aina moja kivyao

Lakini nachohakikisha asubuhi wana cornflakes mchana wanakula shule, wakirudi wana cornflakes, usiku wanakula tunachokula

Kuna wadogo ambao hawaendi shule ndio huo uji na maziwa na supu kama tunapika nyama ya kuku au ya ng'ombe wanatolewa supu, ila usiku na wao wanakula tunachokula (mchana ugali unapikwa though )

Anyway natafuta mpishi mzuri jamani if anyone knows one kindly pm me, am not a good cook either na safari za mikoani zinajaza chakula na matunda na samaki ambazo naona hazitendewi haki kwenye mapishi

Wapi Asha Diiii
 
wana miaka 7 sasa! mmenikumbusha malezi! to GOG BE THE GLORY! natamani kichanga tena, loool
 
asubuhi nawapa twins uji wa lishe ya kutengeneza mwenyewe, huo ni lazima kwao SI OMBI! yaani nahakikisha dada anawanywesha kabla ya kwenda shule, huo uji unakuwa na mchanganyiko wa vitu mbalimbali isipokuwa dagaa, wana allergy na samaki na mayai! kwasababu wamegoma kula wheetabix yenyewe, naimix kwenye uji wakati unachemka, inayeyukia huko! naweka na asali badala y asukari na butter or blueband kidogo! kama tukisaga unga bila karanga, naweka pia peanut butter!

saa nne mpaka saa 7 ni maziwa ya ng'ombe! wanamaliza lita kwa mchana mmoja, na lita usiku. saa 7 mchana ni ugali lazmaaaaaa wale, kama leo na maharage, kesho mchuzi, keshokutwa bamia za nazi, inayofuata kabichi nk, wanalala mpaka 10 au 11, wakiamka ni fruits, kama leo papai, kesho ndizi, keshokutwa machungwa, nimemwambia dada hata kama hakuna tunda siku hiyo wapewe carotts, saa 12 wanatolewa nje for a walk mpaka saa 11 au 12, wakirudi wanakula NDIZI ZA KUPIKA NAZIMIX NA NYAMA YA KUKU WA KIENYEJI AU SAMAKI MARA MOJAMOJA SANA MAANA WANA ALLERGY, KAMA LEO NIKIBLEND, KESHO NASONGA KWA MKONO ILI WAZOEE OL WEATHER, then kuoga! baada ya hapo ni kuruka kwenye viti, kuvuruga vitanda vya watu nk.


by the time ni saa mbili usiku, wana njaa tena wanakula tena food rice, lakini maziwa tunakuwa tumeshapak kwenye chupa zao tayari kwa kulala, in between wanaweza KUnywa soda, biscuits, chama etc!

kabla ya kulala wanapata chakula cha kiroho, sala ni muhimu! HIVYO TUWAKUMBUSHE WATOTO KUSALI KABLA YA KULALA, SI OMBI NI LAZIMA!

Ratiba yako nimeipenda ila inataka uwe na mfuko wenye kina kirefu.
 
Back
Top Bottom