Prisoner of hope
JF-Expert Member
- Aug 9, 2017
- 2,440
- 2,572
Big up ndugu...Kama nilivyokujuza kwenye uzi wangu wa kazi & ajira; nimeanza kufuga nikiwa mtoto; hivyo mayai ya kienyeji nayajua vyema.
mkuu inategemea mayai hayo unahifadhi kwa ajili ya matumizi gani. Wingi wa mayai uliyonayo ni kiasi gani. kama ni matumizi ya kula na ni mengi weka kwenye chumba chenye kiyoyozi (air condition) weka nyuzi joto nne yatakaa mpaka muda wa wiki tatu. kama utahifadhi kwa ajili ya kuangua inapaswa yasizidi siku kumi baada ya kutagwa. nikimaanisha baada ya wiki mbili ubora wake utakuwa ni hafifu. kinachosababisha yaharibike ni kwa sababu yana mbegu ya jogoo
unaweza ukaweka kwenye friji lakini sio eneo la mlangoni. friji nzuri ni inayotoa hewa ya baridi (frost free)
kabla ya kuyahifadhi ni vyema ujue lini yametagwa na lini itakuwa ni ukomo wa kuyahifadhi. nashauri kama unanunua kwa watu tofauti tofauti uyahifadhi kwa kipindi kifupi zaidi maana wakati mwingine ni nadra kujua yametagwa lini kwa uhakika.
hivyo kwa kutumia kifaa chenye mwanga mkali na chumba chenye giza unaweza kuona kama ndani ya yai kuna dalili za kiini kuendelea. google eggs candling uweze kijifunza ni namna gani ya kuifanya. unaweza kufanya kwa yai moja moja au kufanya kwa tray nzima kama umetengeneza kifaa cha kukuwezesha kufanya hilo