Naomba kufahamu namna bora ya kuhifadhi mayai ya kuku wa kienyeji ili yasharibike haraka na nitagunduaje yai lililoharibika

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Posts
2,440
Reaction score
2,572
Habari zenu ndugu zangu...naimani mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku.

Kwanza, naomba kufahamu namna bora, ya kuhifadhi mayai ya kuku wa kienyeji, ili yasiweze kuharibika kwa haraka. Nikiwa na maana ya mazingira yake ya uhifadhi....

Pili, naomba pia kufahamu ni kwa namna gani, mtu anaweza kugundua yai lililoharibika, kabla hata ya kulivunja?. (Hususani yai la kuku wa kienyeji).

Naleta mada mezani, wote mnakaribishwa.....karibuni sana.
 
Utunzaji sijui; lakini namba mbili najua.
Yai la kienyeji lililoharibika ukiliweka kwenye maji linaelea juu wakati yai zima linazama. Njia nyingine ni ile ya kutumia tochi. Yai bovu linaonekana giza ukiliangaza kwa tochi wakati yai zima linaonekana kama rangi ya manjano.
Ahsante mkuu.
 
mkuu inategemea mayai hayo unahifadhi kwa ajili ya matumizi gani. Wingi wa mayai uliyonayo ni kiasi gani. kama ni matumizi ya kula na ni mengi weka kwenye chumba chenye kiyoyozi (air condition) weka nyuzi joto nne yatakaa mpaka muda wa wiki tatu. kama utahifadhi kwa ajili ya kuangua inapaswa yasizidi siku kumi baada ya kutagwa. nikimaanisha baada ya wiki mbili ubora wake utakuwa ni hafifu. kinachosababisha yaharibike ni kwa sababu yana mbegu ya jogoo

unaweza ukaweka kwenye friji lakini sio eneo la mlangoni. friji nzuri ni inayotoa hewa ya baridi (frost free)
kabla ya kuyahifadhi ni vyema ujue lini yametagwa na lini itakuwa ni ukomo wa kuyahifadhi. nashauri kama unanunua kwa watu tofauti tofauti uyahifadhi kwa kipindi kifupi zaidi maana wakati mwingine ni nadra kujua yametagwa lini kwa uhakika.

hivyo kwa kutumia kifaa chenye mwanga mkali na chumba chenye giza unaweza kuona kama ndani ya yai kuna dalili za kiini kuendelea. google eggs candling uweze kijifunza ni namna gani ya kuifanya. unaweza kufanya kwa yai moja moja au kufanya kwa tray nzima kama umetengeneza kifaa cha kukuwezesha kufanya hilo
 
Asante sana mkuu, God bless you.

Back
Top Bottom