Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na huo ndio ukweli kama huna mishe za uhakika ni heri kupambana na fursa zilizopo eneo uliopo Dar maisha ni gharama sana inahitaji uwe na chanzo cha uhakika cha pesaHakuna maisha rahisi,ni lazima upambane ili kutoboa.
Kuna sehemu nyingi tu huwa hazina uswahili, kwa Tz mara nyingi hiyo kasumba huwepo maeneo ambayo hayajapangiliwa vizuri kimakazi au sehemu uliyojaa watu wenye kipato cha daraja la chini.Hivi mbagala kuna sehemu hamna uswahili?
Anyway hata hivyo Tz hamna sehemu isiyo na uswahili labda kama hawa ishi watz hapo.
Mbagala, Kiwalani, Vingunguti au Manzese ni sehemu ziko poa sanaHabari Wana great thinker
Katika harakati za kuwaza nitafanya biashara gani na nikae wapi nimekaa nimefikilia nikaona dar es salaam utakuwa mkoa Bora kwangu Kwa kuanza maisha.
Umri miaka 25 jinsia kiume.
Sina UZOEFU wowote na mkoa huo ila naamini kutobolea hapo sababu zilizonifanya kuwaza hivyo idadi kubwa ya watu pia mzunguko mkubwa wa biashara pia upatikanaji na huduma nyingi za muhimu.
Naomba kufahamu ni maeneo gani ambayo hayana uswahili mwingi wizi mwingi sehemu tulivu kwako wewe na Mali zako Kwa dar na pasiwe mbali na mjini.
Na Kwa uonavyo, je dar ni mji mzuri Kwa kuanzia maisha au Una weza nishauri kama kuna mkoa mwingine mzuri zaidi Kwa kijana mpambanaji.
Afu nizidi changanua mawazo.
Ukisema na gharama za wastani kwa chumba masters itakuwa vizuri zaidi.
Natokea kigoma mkoani.
Natanguliza shukrani kwako mchangiaji.