Humilis
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 889
- 1,070
Huwa inakuja kama instinct fulani tu,na naamini hakungalia upole tu,kuna muunganiko wa vitu vingi ambavyo vingi hawezi kuvielezea lakini upole ndo ikawa rahisi kuuelezea.Mfano kama umeishi na wasukuma kwa muda fulani..ikitokea labda umeenda kwenye jamii ya wangoni,ukiona mtu anayeendana na wasukuma ,kuna hisia itakwambia kabisa huyu anaweza kuwa msukuma.Ukiulizwa kwa nini unaweza jibu ni kwa sababu ya urefu,japo kuna vitu vingi zaidi ya urefu vilivyokupa fikra kuwa huwa huyo mtu ni msukuma.Mkuu nina rafudhi ya kichuga..
Kuna mdada mmoja yopo early 40 kaka yake ni rafiki yangu(kind of) nilikua nikienda hapo kwa kaka yake anansalimia "Habari yako Ambwene" mimi naitika tu always bila kujua.
Siku moja nipo na kaka yake, kaka yake akaniita wewe "Msukuma" njoo hapa yule dada akashangaa kusikia mimi ni msukuma. Akaniambia siku zote alikua anajua mimi ni mnyakyusa kutokana na jinsi ninavyoonekana ndio maana alikua ananiita Ambwene...Kwamba Vijana wa kinyakyusa ni Wapole.