Naomba kufahamu ukweli kuhusu vituo vya tiba mbadala (sanitariun Clinics)

Naomba kufahamu ukweli kuhusu vituo vya tiba mbadala (sanitariun Clinics)

tunage

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
252
Reaction score
168
Wakuu habari zenu,

Kumekua na hivi vituo vya tiba mbadala na ukienda wanatoa huduma ya kupima mwili mzima,

Sasa nahitaji kujua kuhusu hivi vimashine(walioenda wanavijua) wanavokutumia kupima unashika tu bila hata kuchukua sample mwilini ni vinauhakika kweli au ni udanganyifu tu
 
wakuu habari zenu,kumekua na hivi vituo vya tiba mbadala na ukienda wanatoa huduma ya kupima mwili mzima,sasa nahitaji kujua kuhusu hivi vimashine(walioenda wanavijua) wanavokutumia kupima unashika tu bila hata kuchukua sample mwilini ni vinauhakika kweli au ni udanganyifu tu
Ukweli ni kuwa hii ni kekundu kekundu hakuna kipimo kama hicho duniani. Wanachofanya Hawa jamaa ni kuwaibia wananchi na hakuna Tiba ya namna hiyo. Na wala shirika la afya duniani halijaidhinisha kitu kama hicho. Usiooteze muda wako bure
 
Ukweli ni kuwa hii ni kekundu kekundu hakuna kipimo kama hicho duniani. Wanachofanya Hawa jamaa ni kuwaibia wananchi na hakuna Tiba ya namna hiyo. Na wala shirika la afya duniani halijaidhinisha kitu kama hicho. Usiooteze muda wako bure
Mkuu naomba nitoe ushuhuda.
Nilienda kupima kwa hivo vimashine vya kwenye SULE HERBAL CLINIC TANGA MJINI,
, bila kuficha nililiwa 20000/= fedha halali ya kitanzania

Mkuu niliambiwa nina magonjwa kama buku hivii, mara moyo, mara nguvu za kiume mara mishipa ina mafuta sana, mara damu haifiki kichwan vya kutosha, yaani ni matatizo ambayo naamini nisingechukua hata mwezi nakufa,

wakaniandikia madawa kama ya 200000/= , nikawaambia sina hela ngoja niende home nikachukue, nikafika home
Nikaongea na wife , sasa cha ajabu nikashangaa naambiwa nguvu za kiume ila mbona GAME napiga kwa ufasaha bila mbwembwe, ndio tukajua tunaliwa, hawa jamaa sio wazur aisee,

Wanacheza na points of weakness tu, ummenda pale unapimwa ujanja ujanja tu labda utapewa mitishamba ambayo inatou magonjwa mengi alaf hela yako ndio imeisha

My take: vile vimashine ni ujanja ujanja tu , watu wanapigwa
 
Kuna Yule Dr Alikuwa StarTV alikuwa Anapinga Sana Unene Ila Sasa Hivi kanenepa si Mchezo...

Kila Mbongo Anatafuta Njia Za Kutokea
 
Back
Top Bottom