Ukweli ni kuwa hii ni kekundu kekundu hakuna kipimo kama hicho duniani. Wanachofanya Hawa jamaa ni kuwaibia wananchi na hakuna Tiba ya namna hiyo. Na wala shirika la afya duniani halijaidhinisha kitu kama hicho. Usiooteze muda wako bure
Mkuu naomba nitoe ushuhuda.
Nilienda kupima kwa hivo vimashine vya kwenye SULE HERBAL CLINIC TANGA MJINI,
, bila kuficha nililiwa 20000/= fedha halali ya kitanzania
Mkuu niliambiwa nina magonjwa kama buku hivii, mara moyo, mara nguvu za kiume mara mishipa ina mafuta sana, mara damu haifiki kichwan vya kutosha, yaani ni matatizo ambayo naamini nisingechukua hata mwezi nakufa,
wakaniandikia madawa kama ya 200000/= , nikawaambia sina hela ngoja niende home nikachukue, nikafika home
Nikaongea na wife , sasa cha ajabu nikashangaa naambiwa nguvu za kiume ila mbona GAME napiga kwa ufasaha bila mbwembwe, ndio tukajua tunaliwa, hawa jamaa sio wazur aisee,
Wanacheza na points of weakness tu, ummenda pale unapimwa ujanja ujanja tu labda utapewa mitishamba ambayo inatou magonjwa mengi alaf hela yako ndio imeisha
My take: vile vimashine ni ujanja ujanja tu , watu wanapigwa