Naomba kufahamu utaratibu wa pensheni kwa watumishi wa umma hasa Mawaziri baada ya kutenguliwa nafasi zao

budagala

Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
75
Reaction score
137
Masaa machache yaliyopita, nimeona baadhi ya mawaziri waandamizi na wakurugenzi wakitenguliwa nafasi zao.

Swali langu: Je, viongozi wa umma nao huwa wanalipwa fao la kukosa ajira kwa kipindi cha miezi 6? Baada ya miezi 6 hawalipwi chochote hadi baada ya miezi 18 ndipo huchukua pensheni zao zote?

Naomba kusaidiwa sababu kuishi bila kipato kwa miezi 18 sio jambo rahisi na ni uonevu mkubwa kutoka mashirika yetu ya hifadhi za jamii.
 
Pole sana mheshimiwa kwa kutenguliwa
 
Akitenguliwa uwaziri haimaanishi na ubunge wake unakoma... Bado anaendelea kula jasho letu la kodi kiroho safi kabisa huku akiendelea kugonga meza kwa mbwembwe....


Kuhusu wakurugenzi hilo sina uhakika nalo, acha niwaachie wakubwa watujuze...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…