Naomba kufahamu

Don chul Lingula

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Posts
363
Reaction score
276
Jamani wanajamii forum naomba kujua eti msanii unapoitwa kwenye interview kwenye media kula hela unalipwa? Mfano kama Diamond alivyoitwaa clouds kuzungumzia inshu ya mtoto Wake kwa Hamisa
 
Hilo swali najiulizaga pia,,,akienda interview ye ndo analipia au analipwa?? Na hata kutambulisha wimbo wanalipa?? Sielewagi
 
Mkuu ingekuwa vyema uka-google
ilo swali, kwa Mimi sina utaalam nalo.
ukipata majibu kumbuka kuleta mrejesho
 
Jibu ni rahisi sana.

Msanii anapoitwa kwenye interview inategemea ameendaje, mfano, diamond platnumz ameitwa kwenye interview Jana na kituo cha media ni kubwa ambayo ni clouds FM, nikimaanisha kubwa kwa sababu inajulikana karibia afrika ya mashariki na hata Tanzania nzima pekee,

Kwa hiyo anapoitwa ina maana ni bure hawawezi kumlipa wala yeye hatoi pesa, kwa sababu tayari ni msanii mkubwa Mwenye jina kila kona ya bara la afrika ndiyo maana anayo haki ya kufanya maamuzi yafuatayo,
1. Kukataa kwenda kwenye interview.

2. Kuomba kulipwa kiasi kadhaa cha pesa kwenye hiyo interview.

3. Kuomba kuwalipa hao media baada ya interview,

Kulipa interview ni pale msanii anapokuwa mchanga na anahitaji kujulikana kimataifa, au kitaifa ndiyo anaweza kulipa pesa ili afanye interview na nyimbo zipigwe kila mara redioni na runingani,

Ukiona msanii mkubwa ameitwa kwenye interview ujue media wamemkubali na hawatoi pesa yeyote, wala hawamlipi pesa yeyote.

Labda ukute kituo / media haijulikani na wanahitaji kujulikana hapo watamchukua msanii mkubwa wanamlipa wakimchukua msanii mdogo hawamlipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…