Naomba kufundishwa Kiswahili chenye maandishi ya Kiarabu

Naomba kufundishwa Kiswahili chenye maandishi ya Kiarabu

Bakari China

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
254
Reaction score
588
Kama tujuavyo, Kiswahili husifiwa kama lugha ya rasmi ya Tanzania. Lakini kabla ya kusanifishwa, Kiswahili kilikuwa kimeandikwa kwenye herufi ya Kiarabu kwa muda mrefu sana. Naomba kuwauliza ninyi wapendwa wenzangu wa JF, nani mtaalamu wa lugha anaweza kunifundisha Kiswahili kilichoandikwa kwenye maandishi ya Kiarabu?

Nahitaji kukisoma kitabu chenye umri zaidi ya miaka 100, lakini nimeshindwa kuelewa kinachosema. Hebu mtaalamu yupi anisaidie! Shukran
 
Picha ya maneno kutoka kwenye hicho kitabu
IMG_20210120_022712.jpg

Siyo kutoka kitabu chenyewe, lakini ni maneno ya kiswahili kinachoandikwa kwenye herufi ya kiarabu(picha kutoka kwa mtandao)
 
sio quran. mmoja anayejifunza lugha ya kiarabu hakuweza kuyasoma kaniambia ni Kiswahili chenye maandishi ya kale.
Kwamba hicho ni kiswahili na sio kiarabu???

Huyo aliyekuambia ni Mtafiti wa Lugha kutoka wapi?

Wewe umeona hapo kuna irabu hata moja ya Kiswahili?
 
Kwamba hicho ni kiswahili na sio kiarabu???

Huyo aliyekuambia ni Mtafiti wa Lugha kutoka wapi?

Wewe umeona hapo kuna irabu hata moja ya kiswahili?
Kwa mujibu wa mwalimu wetu, Kiswahili kilikuwa kimesanifishwa na kubadilishwa kuwa maandishi ya kirumi(latin alphabets) na mamlaka ya ukoloni wa Uingereza, mnamo 1930s. Kabla ya hapo, lugha hiyo ilikuwa huandikwa kwenye herufi ya kiarabu. Alphabet ya kiarabu ilitumika kuandika Kiswahili kuambatana na matamshi yake.
 
Kwamba hicho ni kiswahili na sio kiarabu???

Huyo aliyekuambia ni Mtafiti wa Lugha kutoka wapi?

Wewe umeona hapo kuna irabu hata moja ya kiswahili?
Sasa tunatumia herufi ya kirumi(latin alphabet, kama vile a,b,ch,d) lakini kabla ya miaka 100, herufi ya kiarabu ا ب ت ilitumika kuandika Kiswahili.
 
sasa tunatumia herufi ya kirumi(latin alphabet, kama vile a,b,ch,d) lakini kabla ya miaka 100, herufi ya kiarabu ا ب ت ilitumika kuandika kiswahili.

Kweli elimu haina mwisho, hili suala sijawahi kulisikia la herufi za kiarabu kuandika Kiswahili.

Anyway, labda upate wana historia wa lugha ya Kiswahili, lakini naona utapata ugumu kwa unachokitafuta.
 
Kweli elimu haina mwisho, hili swala sijawahi kulisikia la herufi za kiarabu kuandika kiswahili.

Anyway, labda upate wana historia wa lugha ya kiswahili, lakini naona utapata ugumu kwa unachokitafuta.
Ndiyo, nasikia kuwa baadhi ya wazanzibari wanaelewa Kiswahili kama hicho, hata nembo ya Chuo Kikuu cha Zanzibar ina herufi hizo. Je, huku kuna mzee mzanzibari anayeweza kunisaidia?
2596006_images.jpg
 
ndiyo. nasikia kuwa baadhi ya wazanzibari wanaelewa kiswahili kama hicho, hata nembo ya Chuo Kikuu cha Zanzibar ina herufi hizo. Je, huku kuna mzee mzanzibari anayeweza kunisaidia?
View attachment 1681760

Ngoja tusubiri wadau wengine, maana wazee wenye huo uelewa kuwapata mitandaoni siyo zoezi dogo, kama wapo kweli.
 
Kwamba hicho ni kiswahili na sio kiarabu???

Huyo aliyekuambia ni Mtafiti wa Lugha kutoka wapi?

Wewe umeona hapo kuna irabu hata moja ya kiswahili?


Huo utenzi wa Kiswahili katika maandishi ya kiarabu.
 
kwa mujibu wa mwalimu wetu, kiswahili kilikuwa kimesanifishwa na kubadilishwa kuwa maandishi ya kirumi(latin alphabets) na mamlaka ya ukoloni wa uingereza, mnamo 1930s. Kabla ya hapo, lugha hiyo ilikuwa huandikwa kwenye herufi ya kiarabu. alphabet ya kiarabu ilitumika kuandika kiswahili kuambatana na matamshi yake.



✔✔✔✔✔✔
 
Back
Top Bottom