Naomba kujua Adam na Hawa walizikwa wapi, Je kuna ushahidi wowote?

Naomba kujua Adam na Hawa walizikwa wapi, Je kuna ushahidi wowote?

AI tata

Member
Joined
Aug 7, 2026
Posts
65
Reaction score
110
Nimekuwa nikijiuliza sana. Adam na Eva walizaa watoto, hata wale watoto wake aliyemuua mwenzake kunguru akatokeanakaonyesha kufukia, kwa vyoyte vile taarifa za walipozikwa ziliendelea kufuatia vizazi na vizazi kuna mjuzi yoyote anaweza akatoa utambuzi wa jambo hili?

Nchi, bara alipozikwa Adam
 
Kuna watu dunia hii wanakomalia matalaka.!?

Eti kisa Kuna cheti cha ndoa.!

Sawa.. Huyo Adamu na hawa walifungishwa ndoa na nani.?

Cheti walipewa na nani.!

Sasa kama ni Imani tu.!? Kwanini kila kitu kisiishe kwa imani.!?

Inatakiwa watu wataliki kwa imani na warudiane kwa imani tu. 🤗
 
Hakuna eneo moja la kihistoria linalothibitishwa kisayansi au kiakiolojia kuwa ndipo walipozikwa Adamu na Hawa, kwani vitabu vikuu vya dini havitaji maeneo hayo, ingawa kuna mapokeo mbalimbali yanayotofautiana kulingana na imani za Kiyahudi, Kikristo, na Kiislamu; kwa mfano, mapokeo ya Kiyahudi na Kikristo yanaamini walizikwa katika Pango la Machpelah huko Hebron au kwenye Church of the Holy Sepulchre Yerusalemu ambapo kuna sehemu ya Chapel of Adam!

Wakati mapokeo ya Kiislamu yanahusisha maeneo ya Jeddah au Iraq.
Eneo lote hili linaangukia kwenye imani za kiroho na hekaya za kale badala ya kuwa na ushahidi wowote wa kiakiolojia au kisayansi, huku Sayansi ikieleza asili ya binadamu kupitia mabadiliko ya jeni badala ya mtu mmoja wa kwanza.
 
Ila haya mambo ya imani sometimes....

Sijui kwanini hivyo vitabu vikatuambia mwanzo wao halafu visituambie mpaka mwisho wao.

Ehee walipofukuzwa bustanini Mungu akamwambia Hawa utazaa kwa uchungu, hao watoto wa Hawa ni wakina nani?!
 
Hakuna ushahidi wa kiakiolojia unaothibitisha kwamba kaburi fulani ni la Adam au Hawwa. Tatizo kubwa ni kwamba Adam ni mtu wa nyakati za kale sana, na hakuna mabaki yaliyothibitishwa kisayansi yanayoweza kutambuliwa kuwa yake.

Pia, hata katika Biblia, tunajulishwa kwamba Adam alikufa akiwa na miaka 930, lakini mahali alipozikwa hakutajwi. Vivyo hivyo Qur’an haitaji mahali pa kaburi lake.
 
Ila haya mambo ya imani sometimes....

Sijui kwanini hivyo vitabu vikatuambia mwanzo wao halafu visituambie mpaka mwisho wao.

Ehee walipofukuzwa bustanini Mungu akamwambia Hawa utazaa kwa uchungu, hao watoto wa Hawa ni wakina nani?!
Mungu alipomwambia Hawa kuwa atazaa kwa uchungu, watoto wake wa kwanza kuzaliwa na kutajwa kwa majina katika Biblia ni Kaini, Habili, na Seth.
 
Ila haya mambo ya imani sometimes....

Sijui kwanini hivyo vitabu vikatuambia mwanzo wao halafu visituambie mpaka mwisho wao.

Ehee walipofukuzwa bustanini Mungu akamwambia Hawa utazaa kwa uchungu, hao watoto wa Hawa ni wakina nani?!
Kuna kitabu cha adamu na Eva ( The book of Adam and Eve) pia kuna kitabu cha Yashiri (The book of jasher) vina maana yake sana tu japo ndiyo hivyo tena Baraza la Nicea lilidai ni Apocrypha books ila kitabu cha Yashiri respect sana.
 
Ni vigumu kujua walipozikwa sababu carbon 14 kwenye carbon dating inachukua miaka kama 6,000 kuisha yote na kwenye historia inaonyesha walikuwepo miaka mingi nyuma hivyo ni vigumu kuwajua, ila kidini nahisi inakuwa sio umuhimu kuandikwa walipozikwa sababu vile ni vitabu vya mafunzo na sio kitabu cha historia,
 
Ngano za kale, imani tumeletewa na mkoloni hizi hata wenyewe wengi wameacha kuamini, ukiwa open na kujielimisha utagundua kuna miungu sana kuliko huyu tuliyefundishwa na mkoloni, safari Asia kuanzia India, China,Japan etc kule billions of people wana miungu yao
 
Wanadai kwamba hao jamaa tangu waumbwe wa mujibu wa matukio ya biblia wamefikisha miaka kama 7,000 yaani haizidi hata 10k lakini ushahidi wao haupo, the same way kuna wahusika walioishi miaka hiyo hiyo na wengine zaidi ya hiyo lakini ushahidi wa uwepo wao upo kuanzia mafuvu, maeneo yao ya makazi, michoro na arts mbalimbali walizoacha.

The same way kwa jamii nyingi zilizoishi kipindi kirefu zaidi ya miaka 50,000 B.C, sasa unapokuja kwa hawa religious characters utaona maajabu, hakuna hata punje ya ushahidi wa uwepo wao kuanzia huyo adam, watoto wake mpaka kizazi cha akina Nuhu, ibrahimu, Suleiman na huyoyesu pamoja na mitume wake wa mchongo.

Hata iyo israel feki ukienda utaoneshwa maeneo wanayodai yalikuwa makazi ya waisrael lkn ukija kiutafiti wa kisayansi na kihistoria utagundua kuwa maeneo hayo hayahusiani na historia ya wahusika wa dini, na pia baadhi ya maeneo yaliundwa kwa malengo haya haya ya kudanganya kutengeneza ushahidi feki wa kusapoti uongo wa biblia.

Pia hiyo israel haijawai kuwepo ni ardhi ya juzi tu haina uhusiano wowote na ule mchongo wa israel ya biblia, the same way kwa wafuasi wa Qur'an dini yenu pia inafuata maandiko ya wayahudi ambao waliunda huo ukristo na baadae uislamu ambao nao unabase ktk uongo wa kutungwa.

Wahusika wote wa dini zote hakuna hata mmoja aliyewai kuwepo, ndiomaana inatumika nguvu kubwa kuwaaminisha watu kupitia vitisho na imani pasipo akili timamu ya kuhoji.

Hizi stories za biblia ni copies ya watu wa jamii zilizoishi mamilioni ya miaka kutoka Afrika kabla hao watu weupe hawajajua ustaarabu wo maisha.

Stories halisi kuhusu mtu wa kwanza hazihusiani na huyo Adamu wa kuundwa na dini za watu weupe, maana mtu wa kwanza hakuwa mweupe na hakuishi nje ya Afrika, the same thing kwa hao wanaoita manabiiz mitume wote walikuwa na mashujaa kutoka Afrika waliopambana dhidi ya Uovu, ushetani na ukoloni wa kiroho na kimwili ulioletwa na hao wazazi wa watu weupe pamoja na vizazi vya watu weupe.

Huyo yesu pia ni copy ya shujaa aliyeishi hapa hapa Afrika mamilioni ya miaka na hakuja kuikomboa dunia bali kuwakomboa watu weusi dhidi ya uovu.

Waafrika wanatakiwa kujua kuna wakombozi wengi waliowai kuja pia ktk dini zenu mnaambiwa kuna Kristo mmoja tu ambaye ndie huyo mnamuita Mungu mwana yaani yesu, lkn kiuhalisia ktk ukweli halisi kuna MUUMBA mmoja tu ambaye hausiani na Miungu yote ya kidini, na kuna KRISTO WAWILI ambaye wakwanza alishakuja Afrika kizazi cha zamani na atarudi, lakini kuna KRISTO wa pili ambaye ndie anaefanya watu weusi wengi ktk kizazi hiki watambue uongo wa hizi dini, ndiomaana kuna muamko wa ajabu kizazi hiki watu wanahoji sana undani wa hizi dini sababu kuna mkombozi aliyeleta NURU kwa watu weusi, huu ni mwanzo tu hizi dini zote lazima zitafutika na huu ndio muda.

Historia imeharibiwa kwa makusudi ili watu wasitambue ukweli, dunia ina mengi ambayo yanapaswa kujulikana wazi, lkn ndio hivyo wengi mko bize kufuatilia upuuzi na ujinga ndiomaana mnanaswa ktk hizo dini za uongo.
 
Ni vigumu kujua walipozikwa sababu carbon 14 kwenye carbon dating inachukua miaka kama 6,000 kuisha yote na kwenye historia inaonyesha walikuwepo miaka mingi nyuma hivyo ni vigumu kuwajua, ila kidini nahisi inakuwa sio umuhimu kuandikwa walipozikwa sababu vile ni vitabu vya mafunzo na sio kitabu cha historia,
Carbon 14 iweze kugundua miaka ya mtu wa kale pale Gorduvai Gorge Arusha alipoishi kiumbe wa zaidi ya miaka 100,000 then ishindikane kwa hicho kiumbe cha kusadikika Adam, kiumbe wa juzi tu?
 
Ila haya mambo ya imani sometimes....

Sijui kwanini hivyo vitabu vikatuambia mwanzo wao halafu visituambie mpaka mwisho wao.

Ehee walipofukuzwa bustanini Mungu akamwambia Hawa utazaa kwa uchungu, hao watoto wa Hawa ni wakina nani?!
Stories za kutungwa hizi kutoka ktk biblia, watu hawashituki tu
 
Kama ilivyo Abunuwasi ambapo taarifa zake zipo kwenye hekaya zake tu, Si katika uhalisia.

Vivyo hivyo, taarifa za Adamu na Eva hazipo katika uhalisia, bali kwenye hekaya za Biblia tu.
Vipi kuhusu Qur'an, yenyewe SI Hekaya?
 
Back
Top Bottom