Naomba kujua biashara ya mapochi (hand bag za wadada) ikoje kuna mdau anataka kufanya?

Naomba kujua biashara ya mapochi (hand bag za wadada) ikoje kuna mdau anataka kufanya?

Laozi Lao Tzu

Member
Joined
Dec 22, 2019
Posts
18
Reaction score
30
Kuna mdau ameniomba nimuulize humu. Anataka kufanya biashara ya mapochi (purse or handbag)

So anataka kujua kama wapo wanaofanya je:-

1) Soko likoje?
2) Aina Gani ya ma bag yanapendwa sana na wadada au wamama
3) Je, wap anaweza nunua mzigo hapa Tanzania awe anauza?
4) Mtaji wa shilling ngap minimum at least wakuanzia?
5) Na mengineyo kama mnaweza kuongeza ongezea kumshauri?
 
Yeye Hana simu ya wasapu???
Mapochi inategemea na location ya anapotegemea kufanyia biashara! Anawauzia watu WA Aina gani,vipato vyao vikoje?
 
Akijichanganya aweke sehemu wamama wa nyumbani wengi jau,nimefungua duka sehemu hiyo yanakaa hatari
Chief samahani, nauliza leseni yako ya kuuza mapochi umekata kama kuuza mabegi au kuuza urembo? Maana nataka kukata leseni ya mapochi lakini sielewi nichague kipengele gan
 
Kuna mdau ameniomba nimuulize humu. Anataka kufanya biashara ya mapochi (purse or handbag)

So anataka kujua kama wapo wanaofanya je:-

1) Soko likoje?
2) Aina Gani ya ma bag yanapendwa sana na wadada au wamama
3) Je, wap anaweza nunua mzigo hapa Tanzania awe anauza?
4) Mtaji wa shilling ngap minimum at least wakuanzia?
5) Na mengineyo kama mnaweza kuongeza ongezea kumshauri?
1. Soko likoje..
Soko la mapochi (handbags & purses) lipo sana, hasa mijini na maeneo yenye wanawake wengi wanaofanya kazi, wanafunzi wa vyuo, na wafanyabiashara. Ushindani ni mkubwa, lakini pia mahitaji ni ya kudumu, kwa hiyo ni biashara yenye mzunguko mzuri wa fedha.

2. Aina gani ya mabegi yanapendwa?*
  • Crossbody bags; Wadada wanapenda kwa sababu ni rahisi kubeba.
  • Clutch; Kwa matumizi ya sherehe..
  • Branded inspired bags; Mfano: LV, Gucci ,Prada, fendi n.k(fake lakini classy)
  • Pochi za kisasa zenye partition nyingi na zipu zinapendwa na wamama..ata mabinti

3.Je anaweza nunua mzigo hapa hapa Tanzania?
Ndio, anaweza kuanza na Kariakoo (DSM) – mabegi mengi ya jumla yapo hapo, kutoka China, uturuki, Dubai n.k. Bei nyingi jumla zinaanzia 6000 kwa pochi za mkono, 15000 min bags, 25-37 pochi kubwa nyingine mpaka 40 Kwahiyo zinatofautiana hizi pochi kwa quality au ukubwa..
- Pia kuna wauzaji wa mtandaoni (Instagram, WhatsApp groups) wanaouza kwa bei ya jumla.. ukifatilia utawaona kina braga and so on..

4.Mtaji wa kuanzia (minimum) wa kuanzia 100,000–300,000 TZS anaweza kupata pochi za bei nafuu kwa jumla na kuuza kwa faida. Hii ni kwa biashara ndogo
- Kwa mabegi ya kiwango cha kati, anaweza kuanza na 500,000–1,000,000 TSh, lakini pia kwa biashara kubwa au mzigo mkubwa pesa itaongezeka zaidi

5. Mambo ya ziada ya kumshauri
  • Aanze na idadi ndogo ili asije akakwamia na mzigo.. na kutazamia eneo alilochogua kama na biashara itakuwa inatoka
  • Afahamu taste ya wateja wake, si kila mtaa unapenda kitu kilekile..
  • Awe na huduma nzuri kwa wateja packaging na delivery vinawavutia.

Akaribie biashara hiyo, ni nzuri kama atajipanga vizuri!
 
Back
Top Bottom