Naomba kujua changamoto za kufunga Turbocharger kwenye gari


Mkuu tutumie logic of how an engine operates. Engine inahitaji Air and fuel mixture (plus spark plugs in petrol engine) kufanya combustion. ECU itapima how much AIr gets in from the intake kisha itaiambia how much fuel to pump.

Tujaalie gari ipo idle, turbo iko on for sure. Unataka kunambia kama hapa kuna more air inaingia kuliko ikiwa haina turbo? Ukinijibu yes, basi una matatizo na turbo setup na intake yako. kwa sababu gari inatakiwa iwe na constant idle position, haijaalishi kama una turbo au huna an average idling rpm ni around 650-700+ but not more than 1000 rpm. Wakati una idle trubo fan ina spin, lakini haipump more Air into the engine, kwa sababu the air is not enough to provide boost. Ndio maana inaitwa turbo lag, kwa sababu katika lower rpms its just spinning not providing boost.

Ujue kuwa Butterfly nayo ni restrictor, unaweza ukapress full gas na isifunguke yote (ikiwa drive by wire), sasa tuseme umekanyaga kidooooogo pedal ya accelerator, butterfly inafunguka kidooooogo kuruhusu hewa kuingia ndani, haitoshi kabisa kuleta boost kutoka turbo ambayo engine ipo 2000 rpm, na ukitaka kujua kama turbo haina effect hapo we pima nguvu ya hewa inayoingia hapo halafu pima bila turbo nguvu ya hewa inayoingia, fungua intake, weka mkono juu ya butterfly wakati gari ipo idle halafu uone nguvu ya hewa inayovutwa bila kuwepo turbo halafu tizama mwenyewe kama kweli turbo ikiwa kwenye 2000 engine rpm ina effect kwenye perfomance. Naamini utafahamu ukifanya practical kwenye hilo.

Engine yenyewe iko so powqerful to suck in Air, ukieka mkono juu ya butterfly halafu ukafanya revving, mkono wako waweza ukazama ndani na ukaumia, hewa inaingia nyingi ya kutosha tu, turbo katika 2000 rpm si kama upepo wa feni tu ukilanganisha na unaovutwa na intake yenyewe?

Umeniuliza kama hio 240HP inakuja hafla bin vuu, mkuu nimesema hapo kuwa kwanza ukiwa rpm za chini hupati 240hp, unajua kwanini? Intake haipokei more air needed to reach that amount of HP. Na katika turbo mkuu, turbine ina spin lakini kama ni low rpms theres nothing, kwa sababu haijapata enough force from exhaust gases to make an effect. Kwani mkuu.

Mfano kama turbine za ndege tu, utaikuta ndege imepark na engine ina spin lakini ndege haiendi, anaanza ku increase throttle ili kuipa enough fuel to start doing its job. Na ndio turbo ilivo, engine ikiwa on turbo is on, lakini haijafikia kile kiwango cha kufanya kazi yake. na turbo si lazima usikie ule mluzi, ule mluzi ndio ujue kama inafanya kazi, turbo inafanya kazi kabla ya kusikia mluzi, mluzi unakuja ikiwa upo kwenye higher rpms ambapo turbo ina spin soo fast.
 

Kuendeleza post ilopita....

Mbadala wa turbo ni Supercharger sasa, hapa naona utapata picha namaanisha nini nikisema turbo ikiwa low rpms it does nothing. Supercharger sasa imeondoa hio kitu lag, kwa sababu supercharger haitegemei pressure ya exhaust gases bali inazunguka na engine inavozunguka, sasa hii ukitia gear tu na kubofya mafuta more air gets in hapo hapo hamna kusubiri. Ukiweka gari yenye supercharger Tujaalie subaru forester.

(mfano tu) ina 240hp turbocharged na forester yengine 240hp supercharged, same weight kila kitu same except hizo Forced induction kits tu, yenye supercharger itaamuacha mwenzake, kwa sababu supercharger itaipa engine boosts kwenye lower rpms wakati turbocharger inasubiri i build up pressure enough to start forcing more air. Wataalamu kuepuka hili wamekuja na anti lag system, ambayo haitegemei exhaust gases to start pumping in more air.

Uzuri wa turbo ni kuwa unaweza kugain more power kuliko supercharger, na turbo ipo efficient because you dont need boost all the time. In case of supercharger you have no choice to stop more air getting in.
 
Ngoja nijaribu kutoa simple explaination may be. Gari ikiwa una drive tuseme nguvu yake bila turbo ina suck in Air labda nguvu 10, nguvu 10 hizi matokeo yake ni 100 HP. wewe umefunga turbo, unataka upate 200 HP, sasa unatakiwa ufunge turbo yenye uwezo wa kusukuma hewa zaidi ya nguvu 10 (labda 20) ambazo engine tayari inazitumia (sio HP).

Sasa hii inakuwa hivi, ukiwasha mashine, gari inatumia nguvu zake 10 kuvuta hewa, ili kuingiza hewa nyingi zaidi, manake turbo yako itumie nguvu 11 ndio itaingia hewa zaidi ndani ya mashine. kwa sababu ikiwa turbo inatumia nguvu 10 na mashine inatumia nguvu 10 hakuna difference ya amount of air inayoingia ndani ya engine, na kwenye turbo its not how quick the air gets in, but how much the air gets in.
 
kwani we unafikiri kama mtu
ana turbo akifika spidi mia afu
yupo gear ya pili, wewe na
same car haina turbo,
utampata?


chilubi nini hiko juu umeandika ha ha ha mkuu acha imagination watu wa mtaani ndo wanapenda kuangalia injini imefungwa nini wakishaona gari ina hata bi-turbo plus intercooler akili zao inakimbia kuliko nyingne yenye turbo moja au mbili lakini haina intercooler

sio hivo jarbu kusoma soma kwanza

tukirudi kwenye hiyo sijui mtu anaturbo afu akifika mia sijui humpati ngoja nkupe mfano unaweza kuta mmoja ana turbo na yuko 100kph but pamoja na turbo yake anAgenerate only 150hp mwngine hana injini ni kavu but 200hp sa hapo who is the best??

tukija kwa 2jz yako hiyo injin ikija kama ilivyo ina hp ndogo labda uiboost lakini sio ikiwa stock afu ianze fatana na kina impreza au lancer afu hiyo 2jz ni stock
 
Turbo Lag: This is the time
between the demand for an
increase in power (the throttle
being opened) and the
turbocharger(s) providing
increased intake pressure, and
hence increased power . Throttle
lag occurs because
turbochargers rely on the
buildup of exhaust gas pressure
to drive the turbine.


chilubi umekopi na ku pestia hapa labda hujaelewa ni hivi mfano unapotaka ovateki au kukimbia ghafla afu ukakanyaga futa boosting haitokei pale pale coz lazma mafuta yaunguzwe hayo uliokanyaga moshi utoke ukazungushe turbine za turbo hewa isafirishwe mpaka kwenye midomo ya cylinder ndo boosting itokee thats turbo lag ule ucheleweshwagi
 
Eminentia,
My god! 😀 ngoja nkuwekee bold katika ulichoquote kwangu then utaona kama wewe husomi vizuri posts na ndo mana huelewi

kwani we unafikiri kama mtu
ana turbo akifika spidi mia afu
yupo gear ya pili, wewe na
same car haina turbo,
utampata?

Mkuu umeona hapo nimeongea same car? sasa vipi wewe na mwenzako mna gari aina ya subaru impreza zote sawa, ila moja ni non turbo nyengine ni turbocharged, vipi ilokuwa non turbo igenerate 200hp yenye turbo igenerate 150hp? nimeongea SAME CAR, tafadhali pitia posts na usome kwa umakini.

Nikakutolea mfano Starlet glanza STOCK turbocharged na Alteza, kukuonesha kuwa just kwa sababu una turbo haimaanishi kuwa una more hp kuliko NA, narudia tena pitia posts usome vizuri.

Mkuu lazima ujue potentiality ya engine yenyewe, watu wana subaru wanafanya swap wanaeka 2jz ama 1jz. engine hizi ukiweka turbo (kitu ambacho subaru models nyingi zina turbo) code inabadilika na kuwa 2jzgte na 1jzgte. If you are not looking to tune your car, yes you can buy Subaru na kusumbuana akina sie tusiotune cars, lakini take both engines and tune them, 2jz ni kiboko. Na ndio maana watu wakifanya engine swap hawaweki boxer engines wala rotary engines, inaekwa 2jz kwa sababu ya potential ilkuwa nayo! the car with stock internals can handle 500+ HP bila kuchange internals wala chochote wewe weka turbo na program your ecu tu basi kwisha, wakati engines nyengine inabidi uchange internals kwa sababu haziwezi kuhimili vishindo vya miripuko not 2jz brother, not 2jz.
 
Eminentia,

Mkuu kucopy sehemu doesnt mean eti sijui maana yake, nimekuletea as a proof, nafikiri hata shuleni ukifundisha 1+1= 2, afu kwenye mtihani ukaulizwa 1+1=? ukijibu mbili utakuwa umekopi? hakuna aliezaliwa akajua how an engine works, au turbo, au computer, we all learn.

Sasa ngoja nkufundishe kitu, Turbo lag has NOTHING TO DO with what you wrote mkuu 😀, kwaio kama gari haina turbo, ikitaka kuovertake kama unavosema yakitokea yaliotokea kama hayo unayoongea tunaita nini? engine lag? butterfly lag? mkuu wacha utani. Imeitwa turbo lag kwa sababu inahusiana na turbo kuchelewa kukick in au kuleta effect, na sio wakati wa kuovertake ni wakati wowote. kutokana na turbo setup yako, turbo itarespond na kuleta effect ikiwa imepata enough pressure from exhaust gases to be able to push in more air than normal vacuum can, unless umefunga anti lag system.

Halafu inaonekana unaichukulia engine very simple ndugu yangu eenh? kwani we unafikiri how long does it take for the smoke to get out of the cylinder? sekunde moja ni nyingi smoke yote inatolewa kwenye mashine.

What happens when you suddenly push the accelerator to the limit, miliseconds actions takes place with the help of ECU. Ukikanyaga mafuta hadi mwisho, ile butterfly (mdomo wa intake) inafunguka yote, which means, more air gets in, when more air gets in, the ecu apo apo ina pump more fuel, ikipump more fuel, it means combustion inafanyika kwa haraka zaidi na kwa nguvu, sasa ukinambia bosting haitokei apo apo sikufahamu, kwa sababu ikiingia hewa nyingi hafla mafuta kidogo, engine ita stall, baada ya kugain boost utapoteza boost kabisa. Na the quicker and powerful the combustion the more power you get, sasa vipi hupati boost? My friend how do you drive your car?

Hebu fanya hivi siku moja, drive kawaida tu kama upo njiani bila kukimbia, mwendo wa 80kph tufanye, then suddenly, suddenly, press the gas to the maximum afu utaona kama hutona gari inakuvuta nyuma. Nini kinatokea hapa? uko 80 umepress hafla, more air gets in, quickly the ecu throw the right amount of fuel, will make the combustion powerful and faster, the gearbox will go down to gear 2 to go hand in hand with engine rotation. yaani ukifanya hivi, kama ulikuwa 80 ikishuka gear 2, trust me, utajikuta unafika 120 faster, sasa hio sio boost imekuja hapo hapo? Dont take the car engine simple ndugu yangu, operation yake ni kitu chengine.

Na katika turbo sasa, kwani we unafikiri uingizwaji wa hewa katika intake nao unafika hata sekunde moja? mana ivo ulivoelezea unataka niamini kama ndio sababu ya turbo kutopata boost hapo hapo. Mkuu ile presha ya exhaust inayokuwa produced wakati unaendesha gari, ina spin turbine ya turbo faster, sio kwamba eti inachukua muda, hapana kabisa. Kama nlivopost juu post moja nikasema unahitaji turbo iproduce nguvu 11 badala ya 10 kama engine.

Turbo ukiendesha speed ndogo tu, inazunguka na inapeleka hewa katika engine, lakini hewa hio inayokwenda kwenye combustion chamber huwa bado not forced air, the same amount gets in, kwa sababu engine yenyewe ina nguvu kubwa kuvuta hewa nyingi tu, sasa turbo kazi yake ni kuingiza hewa ZAIDI ya engine, ili turbo iingize hewa zaidi kuliko engine yenyewe inatakiwa iizidi ile engine otherwise, inakuwa turbo lag ikiwa haiingizi hewa nyingi. Mfano engine kawaida inaingia hewa lita 2 labda, ili turbo ilete boost iingize hewa lita 2.1 zaidi ya ile ya engine, ikipeleka lita 2 kama engine, it means there is no boost kwa sababu inasukumu hewa ile ile inayovutwa na engine, haiongezi kitu
 
Wakati stock intake inatumia nguvu 10 kuingiza hewa ambayo tuseme ni lita 2, turbo izunguke kwa nguvu 10.1+ ili kuingiza more then 2 liters. ikizunguka below that, it means inaingiza same air as stock intake hupati boost hapo.

Na kwa mfano turbo yako inaleta effect katika 3000rpm, na upo around 3000+rpm, hakuna lag hapo, hapo kuna reaching the maximum power tu ndio inachelewa. Kama ilivo gari ikiwa at 6500 rpm ina 240 hp, lakini ukiwa katiks 2000rpm you are only may be 80hp, hii haimaanishi your car has lag, it still generates the power it can at those rpms, the case is different in Turbo
 
naongezea kidogo

engine za petrol hazipitishi upepo moja kwa moja kama diesel engines. unapobuild boost kwa kukanyaga mafuta lets say at wide open throttle, injini inapokea boost yote. unapofanya lift off yani kuachia accelerator throttle body iliyoko kati ya charge pipe (upande ambao turbo inasukuma kwenda kwenye intake manifold ya engine) inafunga. Hapa kwa gari za petrol eg. Subaru sti, glanza V turbo, kuna ile sauti ya chafya "CHYUUUUU" hii ni baada ya boost kukosa pa kwenda hivyo hutolewa na Blow off valve (dump valve).

Nawasilisha wadau
 
Eminentia mi napenda tuwe tunajua mambo ya magari, ni very interesting kwa kweli. Najaribu kukutafutia ma infos kwenye hizi mambo. cheki hii video, we achilia kuwa Is300 imeipiga makwaju turbo subaru, itizame subaru ilivoreact wakati wanaanza kuvutia, hakuna turbo lag hapo na ameondoka faster tu. sio kama vile ulivosema


Tizama na hii walipofanya second run supercharge with no nitrous na turbo charged lexus in yellow, tizama jamaa alivoondoka, hapo tayari turbo imeshaanza kupiga kazi, tizama alivomuacha mwenzake faster. then unambie eti turbo lag kweli?

 
2jz unayoidharau hio ukaona bora boxer

tena iko stock sasa


Eminentia 2jz kwa boxer engine.... I will always choose 2jz... yaani jamaa katangulia na kaachwa, ile milio unayoipenda fyuu fyuuu inalia tu lakini anaachwa, na still jamaa anamwambia atangulie ivi..... you still think boxer can compete with 2jz? 2jz is a monster when it comes to tuning.
 
Wataalamu wa mambo ya magari, nimeomba kufahamishwa hiyo 'turbo' huwa inasaidia nini kwenye injini? na je ina disadvantages zozote kwenye injini?

Naona mnaruka ruka tu as if hamuoni swali langu.

-Kaveli-
In short inaipa gari extra power.
Madhara unaweza kupasua engine block kama ukiifunga funga kienyeji bila kuzingatia characteristics za injini husika.
Engine nzuri kufunga turbo ni Toyota 1Jz au 2jz
Subaru engine Zake zote zinakubali tuning bila matatizo.
Mk series VW
Nissan skyline gtr
Mitsubishi Evo
Toyota supra (nimesahau aina ya engine yake) Hii Ina balaa baya ikifanyiwa tuning.
 
chilubi,
Mkuu ,
Turbo inakuwa on the moment unapowasha engine ,una theory nyingi Sana na maelezo mengi lkn hayako kitaalam , mi naweza yaita ni ya mtaani!

Chukua pressure gauge , then pima kwenye inlet manifold uone Kama itakuwa ni atmospheric pressure, , jibu utapata kuwa Kuna zaidi ya hiyo pressure ,mind you kuwa engine compression stroke hutengeneza vacuum (negative pressure), kwa maana nyingine kipimo kinapoonesha more than atomospheric pressure kwenye inlet manifold ni kudhihirisha kuwa turbo imeshafidia hadi Ile vaccum inayosababishwa na compression stroke.

Idea nzima ya gari za turbo sio mbio Kama unavojadili, Bali ni compact power source , ie displacement ndogo , lkn unapata nguvu nyingi,
Natural aspirated engine huwa zingeweza kuwa na ufanisi sawa na turbocharged engines ila zingekuwa nzito na Kubwa na nzito Sana.

Wepesi unaouona kwenye gari za turbo ni bonus kwa kuwa na engine ndogo ,yenye nguvu na isiyo nzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…